Search This Blog

Thursday, February 28, 2013

MILOVAN AONDOKA BONGO - RAGE AKIMWAGIA LAWAMA KUHUSU USAJILI - CIRKOVIC AJIBU MAPIGO


ALIYEKUWA kocha wa Simba Milovan Cirkovic ameondoka nchini jana alfajili na shirika la ndege ya Uturuki baada ya kufanikiwa kulipwa fedha zake dola 32 alizokuwa anaidai klabu hiyo.

Kocha huyo ambaye alikuja nchini mapema mwezi huu kwa ajili ya kudai fedha zake baada ya kudanganywa na uongozi wa Simba kuwa wanamtamlipa fedha zake bila mafanikio yoyote ndipo aliamua kuja kudai mwenyewe.

Hata hivyo baada ya kusota muda mrefu huku viongozi wakiwa wanampa ahadi kila siku hatimaye jana alfajiri alifanikiwa kuondoka baada ya kulipwa deni lake la Dola 32 kutoka kwa Malkia wa nyuki Rahma Al Kharoos ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha na mfadhili wa klabu hiyo.

Kocha huyo ameondoka na rekodi ya ubingwa Simba ikiwa ni pamoja na rekodi kubwa ya ushindi ‘mnene’ wa mabao 5-0 dhidi ya watani wao Yanga, msimu uliopita.
 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema kuwa uongozi wake haupaswi kulaumiwa kwa kusajili wachezaji wasio kuwa na uwezo bali anayetakiwa kulaumiwa ni aliyekuwa kocha wao Mserbia Milovan Cirkovic.

Rage alisema kuwa wachezaji wote waliowasajili msimu huu ni pendekezo la kocha huyo ambaye alitimuliwa raundi ya kwanza baada ya timu kutofanya vizuri katika michezo yake ya mwisho.

Alisema awali waliwaleta wachezaji wawili kutoka Cameroon lakini kocha aliwakataa na kuwasajili wachezaji wake ambao aliwataka yeye.

Aliongeza kuwa haoni sababu ya wao kulaumiwa kwa sababu wao ni uongozi na sio wachezaji na kuongeza kuwa kama watu wanawalaumu wao wanacheza namba ngapi uwanjani.

Rage akiwa anatoa kauli hiyo tayari kocha Milovan kwa upande wake alikwisha sema kuwa katika wachezaji ambao alitaka wasajiliwe aliyesajiliwa ni Mrisho Ngassa pekee na wengine uongozi ulishindwa.

Msimu huu simba iliweza kusajili beki Lino Musombo, Kanu Mbiyavanga (Congo), Patrick Ochierg (Kenya) na Komabil Keita (Mali).

Lakini baadaye waliwaacha wachezaji watatu na kumbakiza mmoja Keita kwa madai ya kushindwa kuonyesha uwezo mzuri katika timu yao.

9 comments:

  1. mi nawashangaa mnaozid kujadili upuuzi wa rage na kaburu

    ReplyDelete
  2. huyo rage aache ubabaishaji, milovan aliwajua wapi wakina ochieng mara ngapi viongozi wana force kupangia timu kama kule morogoro kocha kamuweka benchi kaseja kaburu anamuambia kaseja avae jezi toka jukwaani akacheza kama wao kina rage ni makocha si wafundishe wao?...uongozi mbovu mara mia hata wakati wa dalali ujinga mwingine kama huu haukuwepo.

    ReplyDelete
  3. Rage hizo fix baba usitudanganye kuwa usajili wote ni mapendekezo ya kocha.
    Nakubali kuwa Ngasa ndio pendekezo la kocha .
    Kubalini udhaifu wenu katika kuongoza timu si kila siku lawama mnazipeleka kwa makocha na wachezaji tu.
    Kiukweli uongozi wenu haujui nini cha kufanya ili timu ipate matokea mazuri.

    Ukitaka mwanao afaulu vizuri mitihani yake muandalie mazingira bora na kumpa kila kinachohitajika na kumfuatilia kiukaribu zaidi.

    Unaposema we unacheza namba ngapi tukueleweje?

    ReplyDelete
  4. simba kitu gani wacha washushiwe vipondo tu na huko angola kapu la magoli lina wasubiri mkija mje kimya kimya simba kageuka panya ha ha ha ha

    ReplyDelete
  5. Rage hawezi kukwepa lawama kwa Simba kuwa ilivyo sasa! kama hachezi anafanya nini kuona simba haifanyi vizuri yeye akiwa kiongozi overall wa timu nzima? ni nani aliliwa kekundu kwenye usajili wa Mbuyu twite ni kocha au yeye huko Rwanda? Aache mambo ya siasa klabuni! Amewekwa hapo kuiwezesha timu ifike tunapopataka! Sasa kwa kuwa hachezi namba yoyote uwanjani matokeo ya sasa ya Simba ni halali? sikutegemea kauli ya aina hii kwa kiongozi wa juu aliyebebeshwa dhamana ya kuongoza klabu kubwa kama simba! Na kama hachezi yeye basi hata Angola tujiandae kwa matokeo mabaya zaidi hadi yeye atakapoingia uwanjani kucheza! Kama si faini kubwa Simba isingeenda Angola kwani ni kuambulia aibu tupu! Nawaalika wenye timu yao kwa kufuata utaratibu uliowekwa kuinusuru timu nafasi ikitokea! Tusifanye kosa! uongozi wa aina hii kukwepa kuwajibika hautufai! Naomba kuwasilisha. NURU SPORTS MSM.

    ReplyDelete
  6. Rage na Kaburu ndiyo maadui wa hasa huyo Kaburu anaifanya Simba kama mali yake binafsi anafanya kama anavyojisikia yaani mmiliki yeye,mwenyekiti yeye,katibu yeye na wachezaji na makocha kama wafanyakazi wake wa nyumbani simba imewashinda wai ache kwa ajili ya kuinusuru kama kweli wanaipenda.

    ReplyDelete
  7. Tatizo linajulikana , soka la tanzania ni ujanja ujanja tu, kuanzia TFF mpaka Vilabu, kwa muda mrefu tumekuwa tuna bahatisha tu, lakini hatuna mipango endelevu. Soka ni biashara na inataka kuendeshwa kwa utaalamu kama kada zingine zenye wataalamu. Embu jiulize afisa masoko wa TFF lini katoa takwimu za kuifanya isitegemee mapato ya mlangoni!!! tunaona wenzetu wakiingia mikataba minono ya kuyafanya mashirikisho yao kusonga mbele. Vilabu vingi havina waataalamu wa kuendesha kisomo, tunaishia kugombania pesa za milangoni.
    Tanzania tuamke tuache ubabaishaji.

    ReplyDelete
  8. mh rage leo unauliza kama unalaumiwa wewe unacheza namba ngapi? kweli umezidiwa si ni wewe uliyesema umegundua wachezaji wa simba hawana stamina, wakati wakiwa chini ya Patrick PHIRI , baada ya kupigwa 5-1 kule Misri, ukaona kocha hafai ukamuondoa na kumleta cirkovic ambaye leo unamtupia zigo la lawama ,nasema hapana tatizo ni wewe.

    ReplyDelete
  9. simba tutafungwa ad milovan arudi au phiri bila ivyo akuna kitu

    ReplyDelete