Search This Blog

Friday, March 1, 2013

MCHEZAJI WA GHANA JOHN PAINTSIL HURU: KESI YA KUMJERUHI MKEWE NA KISU JICHONI YAFUTWA


Mke na jirani wa mchezaji wa kimataifa wa Ghana John Paintsil wote kwa pamoja wameamua kutoendelea na kesi walizofungua dhidi ya mchezaji huyo, polisi nchini Ghana imesema.

Afisa upelelezi Freeman Tetteh alisema Paintsil alituhumiwa kumsababishia majeraha mkewe, Richlove, na pia alimjeruhi jirani yake mmoja huko jijini Accra siku ya ijumaa iliyopita. Lakini afisa hugo wa polisi alikataa kuzungumzia chochote kuhusu ripoti kwamba Paintsil alimtoboa jichoni mkewe na kisu.

Hata hivyo mashtaka note dhidi ya mchezaji hyo yameondolewa dhidi ya mchezaji hugo wa zamani wa  West Ham na Fulham, Tetteh alisema, ingawa polisi imechukua maelezo kutoka mke wa Paintsil na jirani, ambaye ndiye aliyetoa taarifa polisi. Tetteh alisema kwamba 'hakuna anayekataa kwamba kulikuwa na vurugu ndani ya nyumba ya mchezaji huyo. Msemaji hugo wa polisi alikataa kuendelea kutoa taarifa nyingine zozote kuhusu kesi hiyo.



No comments:

Post a Comment