Search This Blog

Tuesday, February 19, 2013

EXCLUSIVE: SIMBA YAPEWA SIKU SABA KUMLIPA MILOVAN LA SIVYO.......

ALIYEKUWA kocha wa Simba, Milovan Cirkovic ameupa siku saba uongozi wa timu hiyo kumlipa fedha zake Sh39mil, vinginevyo atapeleka malalamiko yake Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa).
 
Mserbia huyo ambaye yupo jijini Dar es Salaam, tangu Jumatano iliyopita amesema;
 

"Simba ni timu ambayo nimefanya nayo kazi kwa muda mrefu na pasipo matatizo yoyote. Lakini kwa hali ambayo nimekumbana nayo kwa siku hizi mbili (Jumamosi na Jumapili), nafikiri imenikatisha tamaa kabisa."

Kocha huyo aliyeipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita alisema amekuwa akiwapiga simu ya kiganjani viongozi wa klabu hiyo pasipo majibu.
 

Alieleza kuwa kabla ya kuja Tanzania alifanya mawasiliana na waagiji wake hao wa zamani na kumtaka aje ili waweze kumalizana ikiwa kumlipa haki yake.
 

"Ni jambo la kushtua kidogo. Nafikiri haipendezi hata kidogo kumpigia mtu simu pasipo majibu.
 

Mserbia huyo alisema kwa hali ambayo viongozi wa Simba wameionyesha dhidi yake ametoa siku saba ili klabu hiyo iweze kumlipa fedha hizo, vinginevyo ataishtaki Fifa.
  

Cirkovic aliweka wazi kuwa anaidai Simba Sh39mil, ikiwa ni mshahara wa miezi mitatu, Oktoba, Novemba na Desemba mwaka jana ndio hajalipwa.
 

Kocha huyo alikuwa akilipwa mshahara wa Sh13mil na Simba kwa mwezi kwa mujibu wake.
Hata hivyo, katibu wa Simba, Evodius Mtawala alisema wamepanga kukutana na kocha huyo ili waweze kumlipa haki yake.
 

"Hatuna tatizo naye, nafikiri kwa sasa tupo kwenye mchakato kukutana naye ili tuweze kumlipa haki yake." alisema kiongozi huyo.
 

Kuhusiana na madai ya kocha huyo kuwapigia simu pasipo majibu, Mtawala alipinga kuwa hajawahi kupigiwa simu na kocha huyo na kugoma kupokea.
 

"Hapana. Siwezi kukataa kupokea simu yake. Nafikiri Milovan (Cirkovic) bado tunaheshimu mchango wake." alisema

4 comments:

 1. LIPENI MSHAHARA WA HUYO JAMAA VIONGOZI WENGINE BWANA KWANINI MNATAKA ADI MPATE AIBU NDIO MCHUKUE MAAMUZI

  ReplyDelete
 2. circovic piga pini wajasiliamali hao

  ReplyDelete
 3. Uongozi Wa simba chini ya Rage ni wakitapeli tu,hapo hakuna maendeleo mpaka huyo mwenyekiti ang'oke u

  ReplyDelete
 4. Acha maneno mengi lipeni pesa zake mambo ya hatuna matatizo na Cicorvic si ya kweli lipa haki yake.

  ReplyDelete