Siku moja baada ya kamati ya rufaa ya shirikisho la soka nchini kumuengua mgombea uraisi wa TFF, Ndugu Jamaly Malinzi kutoka kwenye kugombea uraisi katika uchaguzi ujao wa TFF, leo hii wadau tofauti wa michezo wametoa maoni yao kuhusiana na sakata. Mmoja wa wadau aliyepaza sauti kuzungumzia suala hilo ni naibu wa waziri wa michezo, Bwana Amos Makalla.
Akizungumza na Ibrahimu Masoud kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM leo usiku, Makalla alisema ameshangazwa sana na kitendo cha kamati ya rufaa kumuengua Malinzi kwa sababu ambazo ameziita hazina mashiko na zimekuosa ushawishi.
"Mimi kama mdau wa soka na michezo kwa ujumla napenda kusema kuhusu hili bila kupepesa macho kwamba kamati hii imepotoka kwenye suala hili. Hii kamati kwenye hili inataka kujishushua heshima, unajua wakati mwingine unaweza kujishushia heshima kwa gharama nyepesi.
"Sababu walizotoa kumuengua Malinzi zimekosa ushawishi. Hoja walizotoa mimi kama mwanamichezo naona hazina mashiko. Malinzi anakosa vipi uzoefu sasa hivi, huku akiwa kiongozi wa chama cha soka cha mkoa? Alishawahi kuwa katibu wa klabu kubwa kama Yanga kwa miaka kadhaa, pia hi huyu huyu Malinzi ambaye aligombea uraisi wa TFF dhidi ya Tenga wakati huo, sasa iweje kipindi hicho aweze kugombea na sasa hivi ashindwe eti kisa kakosa uzoefu. Uzoefu gani wanauzungumzia ambao alikuwa nao kipindi hicho na asiwe nao sasa," aliongeza Naibu waziri huyo.
"Maamuzi ya namna hii yanadhoofisha kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya Jakaya Kikwete katika kurudisha uzalendo kwenye michezo. Raisi amefanya mengi katika kuhamasisha watu kupenda michezo, sasa hivi watanzania tumeanza kupenda michezo. Tenga ameongoza vizuri na sasa tunahitaji TFF makini itakayokuwa ikiongozwa na viongozi makini watakaoiongoza soka yetu na hatimaye tuweze kwenda AFCON na World Cup.
"Mimi kama waziri wa Michezo ninamuomba Raisi Tenga aliyewateua watu wa kamati hiyo aingilie suala na kuweka sawa, hali isije kuwa mbaya na watu wakaanza kupoteza upenzi na soka kwa mambo ya ajabu kama haya. Viongozi wa kamati kama walitaka tujue na madaraka na uwezo wa kufanya hili walilofanya wamefanikiwa kwa hilo, lakini sasa nawaomba watumie busara. Wasiwafanye watanzania waache kupenda mpira, wasiturudishe nyuma na jitihada za serikali katika kukuza michezo. Nawaomba wamrudishe Malinzi kura zipigwe kwa haki tupate uongozi bora." - alimaliza naibu waziri huyo wa michezo na utamaduni.
MH. MAKALA NAKUSHUKURU KWA KUTOA KAULI HII WATU WENGINE WANATAFUTA KUSHUSHIWA HESHIMA KWA BEI NAFUU HATA KAMA MTU UWE MBUMBUMBU WA KANUNI AU SHERIA KIASI GANI TAFADHARI PAMOJA NA KUMRUDIHSA MALINZI KUGOMBEA TAFADHARI NAOMBA WADAU WA SOKA TUUNGANE TUSHINIKIZE KAMATI NZIMA IJIUZURU TOKA MADARAKANI WASITUFANYE WATANZANIA NI WAJINGA....SAHISHO JINGINE MWANDISHI NIMEMSIKIA MH. MAKALA KATIKA KIPINDI CHA SPORTS EXTRA KAWA MUWAZI KUWA ANATOA MAWAZO NA USHAURI HUO SIO KAMA WAZIRI AU NAIBU WAZIRI BALI KAMA AMOSI MAKALA MCHEZA SOKA NA MPENDA MICHEZO TAFADHARI WALIVYO WADHAIFU KAULI YAKO WATCHUKULIA KAMA SERIKALI KUINGILIA KATI UTASIKIA TAMKO LA BABA YAO KULE ZURICH...!! C UNAMJUA MBABE MWINGINE NA MUNGU MTU DUNIANI ANAITWA BLATTER......!!
ReplyDeleteKAMATI NZIMA ILIYOTOA MAAMUZI JANA NAOMBA IJIUZURU KWANI HATA KAMA KUNA MJUMBE ALIPINGANANAO TULITARAJIA ANGETOA TAMKO LAKE MAPEMA NA ANGEJIONDOA KWENYE MAAMUZI YALE...!! SO HAYO MAAMUZI MABOVU WAWAJIBIKE WOTE "COLLECTIVE RESPONSIBILITY"
Kasema kweli tupu diri walilopanga limetibuka wamebaki na aibu tupu
ReplyDeleteNdiyo maana soka la bongo ni kazi ngumu sana kusonga mbele! Kila siku ni ujinga mtupu unafanyika! Watu wanafanya maamuzi ya ajabu kabisa hata sijui ni kwa faida ya nani. Vilabuni shida, vyama vya mikoa shida na sasa TFF kwenyewe! Hebu angalia upuuzi wa viongozi wa Simba na swala la Milovan, Yanga na Kabange Twite! Huwezi kutegemea viongozi makini kufanya hayo! Ndiyo maana nimeamua kujitenga na soka la bongo!
ReplyDeleteNAIBU WAZIRI AMETOA MAONI YENYE MASHIKO.BINAFSI NILISHASIKIA TETESIAMBAZO SIKUZITILIA MAANANI TOKA SIKU ZA NYUMA KUWA NYAMLANI ALIKUWA ANAANDALIWA KUMRITHI TENGA,NA TETESI HIZO ZILIKWENDA MBALI ZAIDI KUWA ALIKUWA ANATUMIWA NA VILABU VYENYE UWEZO WA KIFENDA KATIKA KUPANGA MATOKEO KWA AHADI YA KUMDHAMINI WAKATI WA UCHAGUZI.SASA NIMEAMINI....BUSARA ITUMIKE,KURA SITOE MAAMUZI
ReplyDeletetruly inakera sana na inauma, kama mdau wa michezo nimegafirika sana na hii kamati ilichomfanyia bwana Malinzi, sijui tunaenda wapi watanzania, mimi nadhani hii nchi ishaharibika kila mtu akipewa maamuzi ya kusimamia kitu fulani, basi anajiona yeye ndiye Mungu mtu, anafanya maamuzi kwa utashi wake yeye bila kuzingatia hata kanuni, very shame upon them.serikali inafanya jitahada kubwa sana ktk kuendeleza mpira ktk nchi ye2 but kuna watu wachache wanaamua tu kwa makusudi kuharibu,very disappointed kiukweli,but nashukuru Waziri mwenye dhamana ya Michezo kaliona hili na kuliongelea, safii!!!
ReplyDeleteAmakweli TFF wanataka kuturudisha kwenye zama zile za Filisi Alafu Tuborongeboronge,,daaa!!kwa hili wamefanya niwakumbuke wagosi wa kaya ndio waliochangia sana kuondoa zile zama
ReplyDeleteInakatisha tamaa......ni ngumu kupata udhamini wa maana kwenye michezo kama hali yenyewe ndo hii.Shaffih wakumbushe kuhusu goal project iliyohusisha nchi 4,senegal,mali na burknafaso na tanzania then fanya ulinganifu wa mafanikio utagundua kuwa tatizo si vipaji,fan base wala investment bali ni planning,cordination n devotion ya uongozi wa soka ktk maendeleo ya soka.naitwa makani.
ReplyDeleteHuu ni ujinga kwa soka la tanzania tumeanza kujenga timu watu wanaweka ubinafsi wao tenga uko wapi na uliwatoa wapi hao wanasheria wasiojua sheria kwenye kamati hiyo,futeni mchakato mzima wa uchaguzi zoezi la kutoa fomu lirudiwe kumbe wameachwa wanasoka bora wa kusimamia michezo yetu kwa ajili ya mikono ya watu,hii tanzania inakwenda wapi jamani.Ushauri wangu mchakato wote wa uchaguzi tff ufutwe uanze mwanzo na kamati zote zifutwe wapewe kazi hiyo hata majaji wasimamie kwani ni muda mfupi ahsante makalla,we ndiye mwanamichezo wa kweli.
ReplyDeleteNawapa pole wale wote walio enguliwa ktk kinyang‘anyiro cha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi TFF..Kwa kawaida kamati zote zinakuwa chini ya wenyeviti wao,na wenyeviti wote lazima watakuwa watiifu kwa yule aliyewateua,cha kusikitisha sana na kukera sana,aliyewateua hadi sasa yupo kimya licha ya madudu yote hayo kufanyika,watanzania wengi walitegemea kusikia kauli ya Rais wa TFF mara tu baada ya kutokea mkanganyiko,kukaa kwake kimya kutazua maswali mengi sana kwa watanzania,lkn kwa hili lilipo fikia hakuhitaji kuundwa kamati ili ichunguze,maana ndio kawaida hasa ya viongozi wa sasa,hasa baada ya naibu waziri kuzungumza juu ya sakata hili,..Ila ni ukweli usiopingika kwamba Rais wa TFF ndiye mtuhumiwa wa kwanza wa sakata hili cz kamati zote zipo chini yake,na kamati zote lazima zipeleke ripoti kwa bosi wao,kuwa kwake kimya kunaashiria hili linalofanyika analijua mwanzo wake hadi mwisho,Tahadhari kwa Rais wa TFF,asome alama za nyakati ili asijivunjie heshima aliyojijengea kwa watanzania..Chukua hatua Rais..
ReplyDeletekamati iliyomtoa Malinzi ilichemsha,isione aibu kula matapishi yao,wamrudishe malinzi agombee
ReplyDeleteNingeshauri mgombea aliyepitwa kugombea kiti cha uraisi naye atangate kujitoa kugombea ili wagombea wajitokeze upya sababu za kufanya hinyo
ReplyDelete.. Yeye kama mgombea kuonyesha kukomaa na hana uusiano wowote na maamuzi ya kamati
.. Watanzania na wapenda mpira wawe na imani naye