Search This Blog

Sunday, January 27, 2013

VIDEO HIGHLIGHT: ADEBAYOR AIFUNGAA VIRAGO ALGERIA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Togo imejizolea alama tatu muhimu hii leo na kuimarisha nafasi yao ya kusonga mbele katika fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika, zinazoendelea nchini Afrika Kusini.
Emmanuel Adebayor
Togo imeilaza Algeria kwa mabao mawili kwa bila katika mechi yao kundi la pili ya kundi D.
Mshambuliaji Emmanuel Adebayor anayeichezea klabu ya Tottenham ya England ndiye aliyeifungia timu yake bao la kwanza, huku bao la pili likifungwa Dome Wome.
Magwiji hao kutoka Magharibi mwa Afrika, kila mmoja wao alihitaji ushindi katika mechi hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupiga hatua, katika mashindano hayo.
Algeria sasa imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano hayo kwa kuwa haina alama yoyote hadi sasa na imesalia na mechi moja katika raundi ya makundi.

No comments:

Post a Comment