Search This Blog

Friday, January 18, 2013

BAADA YA SUAREZ KUKIRI KUJIRUSHA ILI KUPATA PENATI - LIVERPOOL YASEMA ITAMUADHIBU KWA KITENDO CHAKE

BRENDAN RODGERS amembwatukia Luis Suarez baada ya mshambuliaji huyo wa Uruguay kukiri kwamba ajirusha ili kuweza kuipa ushindi timu yake.

Suarez jana alikaririwa na vyombo vya habari akikiri kwamba alijirusha kwenye mechi dhidi ya Stoke msimu huu na kuisadia timu yake kupata penati illiyoipa ushindi Liverpool.

Lakini masaa machache bvaada ya Suarez kukiri dhidi ya vitendo vyake hivyo, kocha Brendan Rodgers amekasirishwa sana, huku akiapa kumuadhibu mshambuliaji huyo.

Rodgers alisema: “Nadhani sio sahihi na haikubaliki. Nimeongea na Luis na suala hili litashughulikiwa na klabu.

“Kujirusha sio kitu ambacho tunaweza kukivumilia, maadili yetu yapo sahihi."

Suarez jana kupitia mahojiano yake na  Fox Sports Argentina alikaririwa akisema: 'Natuhumiwa kuwa najirusha sana kwenye mechi tena hasa kwenye eneo la hatari. Walisema hivyo tulipocheza na Stoke City, kwa siku ile walikuwa sahihi. Nilijirusha ili kupata penati kwa sababu nataka timu yangu ishinde."

2 comments:

  1. Suarez aliongea mengi sana si hilo, weka na yale mengine ili wadau ambao hawakupata kusoma alichoongea wajue usiwe wa upande mmoja that's not football!

    ReplyDelete
  2. ni kweli kabisa toa yote acha kung'ata upande mmoja

    ReplyDelete