Search This Blog

Saturday, January 19, 2013

AZAM YAANZA KWA KIPIGO KENYA - YACHAPWA 2-1 NA AFC LEOPARDS

Timu ya soka ya Azam leo imepokea kipigo cha kwanza katika ziara yake huko nchini Kenya. Azam ambayo hivi karibuni walitetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Tusker ya Kenya, leo walicheza na AFC Leopards katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi na wakafungwa 2-1 huku wachezaji wao wawili Atudo na Mcha Vialli kukosa penati mbili walizopewa ndani ya dakika 90 za mchezo.

No comments:

Post a Comment