Search This Blog

Friday, December 21, 2012

TETESI - WIKI MOJA BAADA YA KUBADILISHIWA MASHTAKA - LULU AACHIWA KWA DHAMANA KWENYE KESI YA MAUAJI YA KANUMBA

Chama cha umoja wa waandishi wa habari kimeripoti kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.


Mtandao haujaweza kuthibitisha taarifa hizi kama ni za kweli...........

7 comments:

  1. Wameanza,hivi kuna watu wangapi wanaozea ndani kwa makosa kama haya??????????Why Lulu na sio wao???????????????????????????

    ReplyDelete
  2. watanzania tunahitaji mabadiriko ya fikra, tunapokurupuka kulaum tu,ni yupi ambae unamfaham kesi yake kaganda magereza?.ikumbukwe lulu ni maarufu hivyo nilazima habari zake uwenazo, huyo unaemjua huko ulipo nani anamjua?. si kila jambo ni la kulaumu lalaum tu.

    ReplyDelete
  3. Hizi ndio sheria zetu, daima magerezani kutakuwa ndio nyumba za masikini na hohehahe, ningeona ajabu huyu binti muuaji pamoja na umaarufu wake aendelee kukaa jela! uliona mara tu baada ya kuua taasisi na watu mashuhuri mbalimbali walivyojitokeza kutaka kumtetea. Geuza upande wa pili wa shilingi laiti kama mauaji yale yangefanywa na mtu mwingine (hawala yake) dhidi yake ungeviona hivyo vyombo vya haki za binaadam na wanaharakati ungesikia huu ni ukatili wa kijinsia na tendo hilo lingechukuliwa kuwa ni mfano katika kuzipa nguvu hoja za unyanyasaji wa kijinsia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kanumba na lULU Ni Yupi Tajiri kuliko mwenzake na mmesahau kuwa mtoto haolew

      Delete
  4. mahakama si mawazo ya mtu kasikia kwa watu, ushahidi na taarifa muhimu ndizo zinazofanyiwa kazi.

    ReplyDelete
  5. ila kwa shria ya tz kosa la kuuwa bila kukusudia linadhaminika hivyo i haki yake lulu kuachiwa kwa dhamana namtakia maisha mema uraiani natumaini amejifunza kitu.

    ReplyDelete
  6. Tuache ushabiki jamani hv ni nani alikuweko huko chumbani wkt yote yanatokea?hamdhan ht lulu angeweza kufa,kwa nini tunataka kulazimisha lulu tu ndie aonekane kakosea?mi naamin yote yanayotokea ni matokeo yaliotengenezwa na mazingira,pombe+mapenzi ndio matokeo ya mchz kuvuta,kila ki2 ni sumu kikitumiwa vby ht asali na utamu wake ukizidisha inakuua.

    ReplyDelete