Search This Blog

Tuesday, December 4, 2012

UGANDA KUIKABILI KILI STARS KWENYE NUSU FAINALI.

 Wachezaji wa timu ya Uganda wakishangilia goli lililofungwa kipindi cha kwanza wakati wa mchezo wa robo fainali ya nne dhidi ya Ethiopia ya michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela, Nambole nchini Uganda.Uganda imefanikiwa kuingia kwenye nusu fainali baada ya kuifunga Ethiopia mabao 2:0
 Mshambuliaji wa timu ya Uganda Robert ssentongo akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa robo fainali ya nne ya michano ya Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Ethiopia uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Nambole nchini Uganda.
Ssentongo ndiye aliifungia Uganda bao la pili na la ushindi.
Mshambuliaji wa timu ya Uganda, Hamis Kiiza akiruka kiatu cha beki wa timu ya Ethiopia wakati wa mchezo wa robo Fainali ya nne ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Nambole nchini Uganda.

1 comment:

  1. Kaka big up sana kwa kilimanjaro... nadhani kwa mchezo wa Waganda wapo juu yetu lazima kukubali... ila mwalimu inabidi achezeshe viungo wengi kama juzi nadhani itasaidia kuwapunguza kasi kimchezo then tukiwatumia wakina Ngassa kwenye counter itakuwa safi sana...
    Kaka mimi kama mfuatiliaji wa blog yako ningependa kukushauri uirekebishe. Kufungua links kunapoteza flow ya kusoma... Kama ungeweza publish kila kitu kwenye page moja bila kuweka links kama ilivyokuwa zamani na bogs kama za Millard ama michuzi....

    MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI KILI STARS & ZANZIBAR HEROES

    ReplyDelete