Search This Blog

Monday, December 10, 2012

KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS: SELEMBE HAJAITWA - MCHA KHAMIS NDANI

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.

Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.

Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).

Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA STARS
Kocha Mkuu wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.

Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.

MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA KESHO
Michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho (Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.

Viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.

Timu hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.

Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.

Mechi za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2 asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).

Kundi C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.

9 comments:

  1. Kevin Yondani (Simba)?

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa unazi unamsumbua sana; nakumbuka sakata la yondani alilishikia kidedea sana; ujuaji, majungu na unafiki havitoendeleza soka la bongo kamwe!

    ReplyDelete
  3. jamani tafadhali bhana, mnaandika kwa uzoefu au ni nini? lelvin yondani Simba, kweli au mnataka watu waongee!! kelvin yondan YANGA AFRICA

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe mwenyewe umekosea eti lelvin yondani hakuna mchezeaji wa simba mwenye jina hilo labda unamaanisha kelvin yondan...na wewe kuwa makini katika uandishi wako

      Delete
  4. Sitaki kuamini sana ka kalamu ya Shaffih iliteleza!!! Huyu bwana huwa haamnini ka Kelvin kenda Yanga. Wana-sports msameeni bure tu.

    ReplyDelete
  5. Wote walioutwa ktk timu ya Taifa wanastahili,kuachwa kwa Selembe na kuitwa kwa mcha ni sawa kabisa,cz aina ya uchezaji wa selembe wapo wengi kwenye kikosi,ila aina ya uchezaji wa mcha wapo wachache wenye kikosi,Selembe huwa ni mzuri sana pale timu inapokuwa na mpira,lakini huwa c mzuri sana tunapokuwa tunahitaji kukaba,lakini mcha ni mzuri pande zote,timu inapokuwa na mpira na hata inapokuwa inatakiwa ikabe,mcha anaweza kutekeleza majukumu ya selembe,lakini selembe hawezi kutekeleza majukumu ya mcha kikamilifu.

    ReplyDelete
  6. Msitake kumlaumu Shaffih majina yaliyotoka TFF na ya Taifa Stars yameonesha kuwa Kelvin Yondan(Simba)..ilikosewa huko huko TFF na si Shaffih

    ReplyDelete
  7. Copping and pasting jaman.....
    matatizo ya kiufundi hayo.

    ReplyDelete
  8. wakati mwingine nasi wasomaji tuwe waungwana natuache kumlaumu mwandishi eti ni mnazi wa timu fulani wakati nasi tunatumia unazi huo huo kulaumu, cha msingi ni kwamba pale (Kelvin Yondani (Simba)) kuna kosa la kiuandishi..wote tunajua kuwa Kelvin Yondan (Yanga). cha kushauri ni kwamba msahihisha maandishi na mhariri wafanye kazi yao kwa umakini

    ReplyDelete