Search This Blog

Sunday, December 2, 2012

AZAM YASAJILI BEKI MWINGINE KISIKI - KWENDA DRC KUJIPANGA NA KOMBE LA SHIRIKISHO

David John Mwantika, beki kisiki wa Tanzania Prisons anakuwa beki wa tatu kusajiliwa na Azam FC baada ya Malika Ndeule na Omary Mtaki, hawa wanaungana na Uhuru Selemani na kufanya jumla ya wachezaji waliosajiliwa na Azam FC kufikia wachezaji wanne.

 Azam FC inatarajia kuelekea Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 13 hadi 23 December kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii (Charity Cup)

Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DCMP na AS Vita Club timu kutoka nje ya kongo kama Azam FC, Tusker FC, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs na Congo Brazavile yatatumika na Azam FC kama maanadalizi ya Confederations Cup

Azam FC inahitaji maandalizi na mechi nyingi za kirafiki nje ya Tanzania ili kupata uzoefu kabla ya kushiriki Confederations Cup. Kwa maana hiyo hii ni nafasi muhimu sana kwa Azam FC

No comments:

Post a Comment