Search This Blog

Wednesday, November 21, 2012

BECKHAM ATANGAZA KUONDOKA L.A GALAXY BAADA YA MIAKA 6

Siku moja baada ya mabingwa watetezi L.A. Galaxy kuingia kwenye fainali ya pili mfululizo ya MLS, David Beckham ametangaza kwamba fainali hiyo itakuwa ya mwisho japokuwa amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake.
Beckham alisaini mkataba wa miaka miwili mwezi January baada ya kumaliza wa kwanza miaka 5 mwaka uliopita ambapo Galaxy walibeba ubingwa wao kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo. Mwaka 2012, Beckham amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya MLS akifunga mabao 7 na kutengeneza mengine matano katika mechi 28. Lakini wiki iliyopita, tetesi za kumhusu kiungo huyo wa miaka 37 kuondoka kwenda Australiakwenye A-LEAGUE zilianza kusambaa lakini kwa haraka zikakanushwa na msemaji wake.

Sasa akiwa anaondoka Galaxy, uhamisho wa kwenda A-League sasa unawezekana, lakini pia anaweza kwenda kwenye klabu nyingine ya MLS au mahala pengine popote duniani ambapo wanataka kuuza jezi za David Beckham.

No comments:

Post a Comment