Search This Blog

Monday, October 22, 2012

ZENGWE: WACHEZAJI WA PAMBA YA MWANZA WAAZIMA VIATU VYA KUCHEZEA KWA WACHEZAJI WA TIMU ZA MITAANI

Hii ndio Pamba ya zamani iliyofanya vizuri kwenye soka wakati huo. Ni vipi historia itajirudia kwa magumashi yanayoendelea kwenye timu hiyo kwa sasa.


Wakati wadau wa soka nchini tukiwa tunapiga kelele juu ya uendeshwaji mbovu wa soka la nchi hii, mambo yamezidi kwenda hovyo katika kanda ya ziwa jijini Mwanza. 

Moja ya timu yenye historia kubwa nchini Tanzania iliyowahi kupata mafanikio makubwa pamoja na kutoa wachezaji wenye majina makubwa waliosadia soka la nchi kufika hapa lililopo - Pamba ya Mwanza ipo katika hali mbaya na kukatisha tamaa kwa maendeleo ya soka.

Ikiwa katika harakati za kutaka kurudi kucheza ligi kuu ya Tanzania bara, Pamba kwa sasa ambayo ipo katika ligi daraja la kwanza inatarajiwa kuanza kampeni ya kutafuta nafasi ya kurudi VPL kwa kuanza kucheza mechi dhidi Polisi Mara ambazo zote zimepangwa katika kundi C lenye timu kama Kanembwa JKT (Kigoma), Morani (Manyara), Mwadui (Shinyanga),  Polisi Dodoma, Polisi Tabora na Rhino Rangers ya Tabora.





Sasa wakati timu ikiwa katika maandalizi ya kucheza mechi dhidi ya Polisi Mara, uongozi wa klabu hiyo umewaagiza wachezaji waende kwenye timu za mitaani wilayani Ilemela wakaazime viatu vya kuchezea kwa sababu uongozi hauna fedha za kununua vifaa hivyo.


"Ni kweli timu yetu sasa imefikiwa katika hali mbaya sana, wakati wa maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Polisi Mara, tukaomba viongozi watuletee baadhi ya vifaa vikiwemo viatu, wakatuambia uongozi hauna fedha hivyo tuende mitaani kwa wachezaji wengine tukaazime. Hivi kweli timu ambayo tayari ina mdhamini (Konyagi) inawezaje kukosa vifaa muhimu kama viatu vya kuchezea?? Ukizingatia wachezaji hatulipwi mishahara sasa fedha zote zinaenda wapi. Nakumbuka kuna wakati mkuu wa mkoa aliwahi kutoa kiasi cha millioni 9 kwa ajili ya kuisadia timu yetu iweze kupanda, sasa sielewi viongozi fedha wanapeleka wapi? Pia wakati Pamba ikiwa kwenye hali mbaya hata viongozi wa wilaya ya Ilemela ambao moja ya jukumu lao ni kuhakikisha soka la wilaya yetu linapanda kwa kuziongoza na kuzisaidia timu za wilaya kama Pamba wamekuwa hawana msaada kwetu, mwenyekiti Evarist Hagila yeye ndio hana msaada wowote muda wote yupo Dar es Salaam." alizungumza mmoja wa wachezaji wa Pamba ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na majeruhi.

Mku wa mkoa Mwanza akitoa msaada wa fedha taslimu shilingi millioni 9 kwa ajili ya kuisadia Pamba
"Pia sasa soka la Mwanza linazidi kudidimia kwa sababu wachezaji wenye vipaji vya kweli wa hapa Mwanza wameacha kucheza mpira kwa sababu ya siasa za viongozi. Mchezaji ukidai tu haki zako za msingi wanakutimua kwenye timu, wanataka kuabudiwa na kuogopwa, jambo ambalo limewashinda wachezaji wengi hivyo kuamua kuondoka Mwanza kwenda sehemu nyingine au kufanya shughuli nyingine tofauti na soka. Sasa jiulize Mwanza ambayo zamani ilikuwa ikitisha kwenye soka itarudi vipi kwa madudu ya namna hii?"
  

No comments:

Post a Comment