Search This Blog

Friday, October 19, 2012

ZENGWE: UWANJA WA KISASA CHAMAZI NA SOKOINE MBEYA UPI UNAFAA KUCHEZEWA MECHI KUBWA???

Kuna taarifa kwamba ombi la Azam FC kutaka mechi dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye dimba lao binafsi la Chamazi Complex limepigwa chini na TFF kwa madai ya usalama. Kutokana na hatua hiyo klabu ya Azam FC kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Facebook wakatoa hoja kwamba iweje uwanja wenye hali mbaya ya kimazingira na usalama kama Sokoine-Mbeya uruhusiwe kuchezewa mechi kubwa zinazohusisha Simba na Yanga na uwanja wao wa kisasa ukataliwe ku-host mechi hizo??? Je mdau una maoni gani juu ya hili? 

5 comments:

  1. hatukatai kwenda Chamazi,lakini ni kweli uwanja huo unaweza ku accomodate idadi ya mashabiki wa Simba na Yanga??hapo ametoa hoja kwa kulinganisha na mashamba ya mpunga,lakini vipi kuhusu capacity ya hayo mashamba ya mpunga??kama suala ni pitch nzuri hata Karume unafaa kuchezwa Ligi lakini hauwezi kubeba idadi ya kutosha ya mashabiki..mwisho Simba na Yanga zinahitaji mapato kwa hali na mali ili kusukuma mbele mipango yao,inavyoonekana Azam hawahitaji pesa kwa kuwa tayari iko ndani ya umiliki wa Bilionea hivyo basi Yanga na Simba haziko tayari kupoteza mamilioni ya mapato kwa kwenda Chamazi...panueni uwanja,cc tutakuja

    ReplyDelete
  2. Hii ni kukatisha tamaa watu wenye uwezo kama bakhresa amejitahidi kuwekeza katika mpira kuliko hizo kulwa na doto kisha anawekewa vikwazo tff mubadilike mtazibeba simba na yanga mpaka lini?

    ReplyDelete
  3. Ni upuuz kuwaambia azam wapanue uwanja wakt wao hata cha mazoez hawana si jukum la azam kuwatafutia kulwa na doto mapato.. Waachen watumie uwanja wao..

    ReplyDelete
  4. kwa asilimia kubwa Azam wana haki kuomba TFF waruhusu mechi zao za nyumbani kuchezwa chamazi, hata za KURWA na DOTO. hata kama uwanja ni mdogo kiasi gani, si zinatengenezwa tiketi kulingana na idadi hiyo????
    HAPA TFF WANAONA KUTAKUWA NA KAUZIBE KA ULAJI MAANA MACHO YAO YOTE NI MECHI KUBWA TU ILI WAVUNE MAHELA MENGI.
    HAIINGII AKILINI TIMU KUINGIZA ZAIDI YA MIL 390 HALAFU ZINAAMBULIA MIL. 150 TU.
    NDIO MAANA AZAM WANATAKA WAFAIDI MATUNDA YA UWANJA WAO.
    mbona hatujawahi sikia Liverpool wanazuiwa kuchezea Anfield (viti 45,270)kisa mechi yao na Man U inaingiza mashabiki wengi,ambapo wangechezea labda Wembley (viti zaidi ya 85,000)?
    HUO NI UMANGIMEZA WA TFF NA UROHO WA MAPATO.
    Nawasilisha kutoka Iringa.

    ReplyDelete