Search This Blog

Tuesday, October 2, 2012

TFF YAZINDUA RASMI MCHEZO WA SOKA LA UFUKWENI NCHINI TANZANIA.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kwa kushirikiana na Kampuni ya Primetime promotions,wameuzindua rasmi mchezo wa soka la ufukweni nchini Tanzania, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wa TFF bwana Angetileh Oseah ,amesema Rais wa TFF bwana LEODGER TENGA yupo mbioni kuunda kamati itakayousimamia mchezo huo huku kamati yak utendaji ya TFF ikiwa tayari imeubariki mchezo huo.

Naye Mratibu wa mchezo huo kutoka Kampuni ya Primetime Promotions Bwana SHAFFIH DAUDA, amesema mchezo huo unataraji kuzinduliwa rasmi mnamo mwezi desemba mwaka huu kwenye fukwe za coco beach jijini Dar Es Salaam.

 Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo yenye mashabiki wengi kwa sasa duniani kote,bwana Dauda amesema TFF kwa kushirikiana na FIFA wanataraji kuendesha kozi maalum kwa ajili ya makocha na wamuzi wa mchezo huo hapa nchini.

Baada ya mafunzo hayo,ndipo mchezo huo utazinduliwa rasmi mwezi wa kumi na mbili. Kwasasa mchezo huu wa soka la ufukweni unachezwa kwenye zaidi ya nchi 170 duniani kote na tayari umeshajizolea mashabiki wengi kutokana na kushirikisha watu wa rika mbalimbali wakiwemo wapenzi wa soka la kawaida,wanasoka wa zamani pamoja na vijana.


Katibu Mkuu wa TFF Bwana Angetileh Oseah akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mchezo wa soka la ufukweni ( Beach Soccer ), kulia kwake ni msemaji wa TFF Bwana Boniface Wambura pamoja na mratibu wa mchezo huo kutoka kampuni ya Primetime Promotions  Bwana Shaffih Dauda.
Kulia ni Bwana Shaffih Dauda akiwaeleza waandishi wa habari mkakati wa kampuni ya Primetime Promotions ambao ndio waratibu wa mchezo huo hapa nchini.
   Hii ni sehemu ya waandishi wa habari  waliokuepo kwenye uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment