Search This Blog

Wednesday, October 3, 2012

SERGIO RAMOS: "KWANINI NILIVAA JEZI YA MESUT OZIL KATIKA MECHI DHIDI YA DEPORTIVO LA CORUNAO"

Mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos amesema leo Jumanne kwamba alivaa jezi ya mchezaji wa mwenzake  wa klabu hiyo Mesut Ozil ndani ya jezi yake  ili kujiletea bahati katika mechi ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Deportivo La Coruna.

"Ningependa kuweka wazi suala hili na kufanunua vitu kadhaa kabla uongo zaidi haujaenezwa na huku watu wakizidi kuutunga. Mesut ni rafiki yangu mzuri sana na nilimwambia kwamba goli langu la kwanza la msimu nikifunga litakuwa kwa ajili yake." Ramos alisema kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter. "Nilikuwa kuvaa jezi yake kwa ndani huku nikijiamini inaweza ikawa mechi ambayo nitafunga bao langu la kwanza , na sio vinginevyo vyovyote vile."

Real Madrid coach Jose Mourinho leo alimuweka Ramos katika listi ya wachezaji wanaosafiri na timu kuelekea Amsterdam kwa ajili ya mechi ya champions league dhidi ya Ajax kesho Jumatano.


 Katika kuzungumzia taarifa kwamba ana bifu na kocha wake na alivaa jezi ya Ozil ili kumkera Mourinho aliyemtoa Ozil katika mechi ya Deportivo, Ramos alisema: " Nina mahusiano sana na kocha wangu,, yenye uwazi na ukweli," Alitweet mhispania huyo. " Naheshimu maamuzi yake na kwangu mimi yeye ndio kocha bora duniani. Go Madrid."Ramos again insisted he has no beef with his coach.

Mourinho alimpiga benchi Ramos katika mechi ya kwanza ya Champions league ya Madrid dhidi ya Manchester City mapema mwezi uliopita, hali iliyopeleka wengi kuamini wawili hao hawpo kwenye mahusiano mazuri.

No comments:

Post a Comment