NEYMAR ATIMIZA MECHI YA 200 NA SANTOS NA GOLI LA HATARI DHIDI YA TIMU YA RONADINHO
Usiku wa juzi nchini Brazili mchezaji Neymar alitimiza mechi ya 200 akiwa na Santos, na kwa bahati nzuri mechi ya 200 ikawa dhidi ya timu anayoichezea Ronaldinho Gaucho Atletico Mineiro.
Katika kuipa heshima mechi hiyo Neymar akavaa jezi maalum yenye namba 200 mgongoni kwa usiku huo.
Huku Santos wakiwa tayari mbele kwa 1-0 kutokana na goli la Miralles alilofunga sekunde kadhaa baada ya mchezo kuanza, Neymar akaja kushindilia msumari kwenye jeneza katika dakika ya 10 ya mchezo kwa goli safi na la uwezo binafsi akiwapita mabeki kadhaa wa Atletico na kwenda kufunga bao kali, na kuifanya siku yake kuwa nzuri zaidi.
No comments:
Post a Comment