Search This Blog

Wednesday, October 3, 2012

MICHAEL BALLACK; HAKUZALIWA MSHINDI WA KIMATAIFA BALI MSHINDI BINAFSI

. Amepoteza fainali kubwa tano alizocheza

. Wajerumani walimuita mchezaji ‘mlaini’ zaidi 



. Katika timu zote alizochezea alikuwa akivaa jezi namba 13 kasoro moja tu Keiserslautern

Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, Michael Ballack ameamua kustaafu rasmi kucheza soka baada ya kulitumikia kwa mafanikio makubwa. Ballack ambaye alipata jina kubwa mwaka 2001/ 02 akiwa kiungo kinda ‘mpiganaji’ katika dimba la Bay Arena na klabu yake ya utotoni Bayer 04 Leverkusen na kuoingoza timu hiyo kucheza fainali ya ligi nya mabingwa mwaka 2002 dhidi ya Real Madrid m,waka 2002 na kupoteza kwa kulala kwa mabao 2-1.

Baada ya mafanikio hayo akiwa na klabu, Ballack ambaye ndiye kiungo aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya nchi hiyo, akiwa amefunga mabao 34 alikwenda katika fainali za kombe la dunia mwaka 2002 huko Korea Kusini na Japan na kufanya mambo makubwa. Alifunga bao katika kila mchezo wa nchini yake wakati ikishinda kwa tabu dhidi ya Marekani bao 1-0 katika robo fainali, kabla ya kufunga tena bao pekee katika ushindi wa nchi yake dhidi ya waliokuwa wenyeji wenza wa michuano hiyo, Korea Kusini katika nusu fainali lakini alikosa mchezo wa fainali dhidi ya Brazil ambao nchi yake ililala kwa mabao 2-0 baada ya kupata kadi mbili mfululizo za manjano katika michezo ya robo na nusu fainali. Akawa amepoteza fainali ya pili kubwa ndani ya miezi miwili lakini ilimfanya kutambulisha kipaji chake kama mmoja ya viungo wapiga ‘freekick’ bora ambao wamewahi kutokea duniani.

Akicheza kando ya viungo wazoefu kama, Jens Jeremies, Stefan Efenberg, Methmet School katika kikosi cha Bayern Munich mara baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Leverkusen, Ballack alikomaa zaidi kimchezo na kuboresha upigaji wa mipira ya vichwa na kutokea mmoja ya wapiga vichwa bora zaidi wa nafasi ya kiungo hapa duniani, akatwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ujerumani mara tatu ndani ya miaka minne na kuwa mchezaji ‘babu kubwa’. Mara moja akawa nahodha wa nchi yake akiwa kinda wa miaka 24, huku wachezaji kama Oliver Khan wakiwepo kikosini. 


Ballack akaiongoza Ujerumani katika michuano ya Mabingwa wa Mabara mwaka 2005 wakiwa wenyeji na kufungwa tena na Brazil katika fainali kwa mabao 3-2 katika Siku ambayo aliamini anashinda taji la kwanza la kimataifa, baada ya nchi yake kuwa mbele kwa muda mrefu, lakini mabao kutoka kwa Adriano Leite yalizima ndoto zake hizo na kutamka kwa hasira “ Ni bora tusiwe tunaingiza timu yetu uwanjani tunapokuwa tunakutana na Brazil” Ballak aliongea maneno hayo kwa uchungu huku akikata tamaa mbele ya mamilioni wa soka duniani akiwa nahodha wa Ujerumani.

‘ The soft player of German’ kama alivyofahamika mbele ya Wajerumani ambao walikuwa wakiamini japo kiungo huyo alikuwa ni bora lakini alikuwa ni mlaini sana awepo uwanjani na anayekata tamaa mapema. Hakuzaliwa mshindi ndivyo inavyoaminika japo ni mchezaji aliyekuwa na kipaji kikubwa cha kupiga pasi timilifu fupi na ndefu kwa usahihi, alitua Chelsea mara baada ya kushindwa ‘kiabu’ mbele ya Italia katika kombe la dunia mwaka 2006 akiwa nahodha, Ujremani ilifungwa mabao mawili katika dakika za 119 na 120 katika mchezo ulionesha ‘power’ ndogo ya timu hiyo mbele ya Italia, akaishia kuvaa medali ya ushindi wa tatu na kuwa fainali yake ya nne kubwa anapoteza.

Alianza taratibu akiwa Chelsea huku akihesabika mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi hiyo sambamba na mwenzake wa timu hiyo Andry Shevchenko ambao kwa pamoja walikuwa wakipata mshahara wa pauni 130, 000 kwa wiki. Ballack alikataa heshima ambayo alipewa na kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye alimuhitaji sana kiungo huyo wakati anaondoka kama mchezaji huru pale, Munich. Fergie alimuahidi unahodha ‘Myahud’ huyo na mshahara wa pauni 120, 000 kwa wiki lakini Ballack aliichagua Chelsea na kudumu hapo kwa miaka minne huku akishinda mataji matatu ya FA na moja la ligi lakini alipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa Mei 21 jijini, Moscow wakati Chelsea ikilala kwa penati mbele ya United. 


Akaenda kuiwakilisha nchi yake akiwa kama nahodha katika michuano ya Euro 2008 na kucheza soka la kiwango cha juu lakini alipoteza mchezo wa fainali mbele ya Hispania kwa Ujerumani kulala 1-0, na wakati akitajwa kama nahodha mtarajiwa atakayenyanyua kombe la dunia mwaka 2010. 

 Micheal Ballack alivaa medali yake ya mwisho akiwa mchezaji mshindi akiwa na matumaini madogo ya kucheza kombe la dunia mwaka huo kwani katika mchezo wa fainali wa kombe la FA dhidi ya Portsmouth, Ballack aliumizwa vibaya na Kelvin Prince Boateng huo ukawa mwisho wake katika soka la Kimataifa. 

Akaenda zake, Leverkusen kumalizia soka lake na kuwa na mafanikio kiasi katika timu hiyo lakini msimu wake wa mwisho haukuwa mzuri na ulikuwa wa mizozo ya mara kwa mara na kocha wake. 

Usiku wa jana Micheal Ballack aliamua kutangaza kutundika daruga zake katika soka. 

HAYA NDIO MAGOLI 10 YAKE 10 BORA 

No comments:

Post a Comment