Search This Blog

Thursday, October 18, 2012

BREAKING NEWS: YANGA YAMALIZANA NA VODACOM JUU YA RANGI YA NEMBO YAO KWENYE JEZI



Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya kutotumia jezi zenye nembo nyekundu.
Vodacom imefikia hatua hiyo kufuatia Yanga kupeleka maombi yao ya kuomba kutotumia nembo hiyo nyekundu katika jezi zao.
Kufuatia maombi ya klabu ya Yanga kupitia kwa viongozi wake na baraza la wazee, vodacom imeona ni busara kuwasikiliza Yanga maombi yao na hivyo kuamua kuipa nafasi ya kuchagua nembo moja kati ya tatu.
Vodacom imetoa aina tatu za nembo na Yanga inapaswa kuchagua moja kati ya hizi nembo tatu.
Swali kwa mashabiki wa Yanga, ipi nembo nzuri kati ya hizi tatu?

6 comments:

  1. Zote mbaya kwani zina rangi nyeupe ambayo ni ya mnyama pia...... rangi ya Yanga ni nyano na kijani.

    ReplyDelete
  2. je kampun ina hzo rangi or external impressional 2

    ReplyDelete
  3. Je kampun ina hzo rangi or externally impressional

    ReplyDelete
  4. Yanga huva ezi za nano na kijani so nembo yao inatakiwa iweya kijani wakati wamevaa jezi za njano na iwe ya jano wakati wamevaa jezi za kijani, simple

    ReplyDelete
  5. hapo haina ubishi sawa sawa mzigo umetoka kichwani umewekwa begani kwani zote simba hizo

    ReplyDelete