Search This Blog

Tuesday, September 18, 2012

A TO Z YA MAMBO YANAYOMUHUSU MFUMANIA NYAVU RADAMEL FALCAO


A - Atletico Madrid

Falcao kwa sasa anaonyesha ubora katika mji mkuu wa Spain akiwa na klabu ya Atletico Madrid. Tangu amejiunga na timu hiyo  mwaka jana amefunga mabao 42 katika mechi 53 .

B - Bogota

Bogota ni mji mkuu wa nchi anayotoka Falcao Colombia, Facao alihamia katika mji huo akiwa mdogo sana. Bogota ina watu zaidi ya Million 7.

C - Colombia

Falcao alizaliwa mjini Santa Marta, Colombia. Uwezo wake mkubwa wa kutpia kambani ulimfanya aitwe kwenye timu ya taifa akiwa bado mdogo, mpaka sasa ameshatupia mabao 13 katika mechi 39.

D - Dream Team

Ikiwa Falcao atauzwa kutoka kucheza La Liga na kwenda  Premier league ambapo klabu zenye uwezo wa kumnunua na zinazoonyesha nia ya kumtaka ni mbili  Chelsea na City ambao wenyewe wanataka kutengeneza dream team yenye forwad line ya kutisha ya Sergio Aguero, Carlos Tevez na Falcao.



E - EL TIGRE(TIGER)
El Tigre ni jina la utani alilopewa Falcao na mashabiki wa Atletico kwa sababu ya staili yake ya uchezaji yenye kutumia nguvu na akili katika kutumbukiza mipira kwenye nyavu za maadui zao.

F - Father
Baba yake Falcao alimpa mwanae jina la mchezaji wake anayempenda kuliko wote; Paulo Roberto Falcao.  Baba yake Falcao pia alikuwa mwanasoka ambaye aliweza kuichezea timu ya taifa ya Colombia.

G - Goals
Kufunga mabao ndio sifa kuu ya Falcao kwa mashabiki wote wa soka duniani. Katika miechezo 250 alizozicheza vilabu vyake, amefunga mabao 163. Kwa uwiano amefunga bao moja katika michezo 1.5 . Magoli yake ya kimataifa yana uwiano wa goli moja katika kila mechi 3.

H - Hat tricks
Falcao amefunga hat tricks nyingi sana katika mechi zake zote alizocheza, hat tricks moja inaizidi ubora nyingine. Hivi karibuni alikuwa ndio mchezaji wa kwanza kufunga hat trick katika UEFA Super Cup, katika ushindi wa Atletico dhidi ya Chelsea, ingawa uwezo wa kufunga hat tricks ulianza siku nyingi nyuma akiwa nchini Argentina. Hat trick yake ya kwanza ilikuwa katika mechi kati ya timu yake ya River plate na Batafogo mwaka 2007. Hat trick yake ya kwanza barani ulaya ilikuja wakati akiichezea Porto katika Europa League dhidi ya klabu ya Austria Rapid Wien na ya pili ikaja miezi mitano baadae katika robo fainali ya mashindano hayo hayo dhidi klabu ya Russia Spatark Moscow. Baada ya kuhamia Spain, haikumchukua muda mrefu kuanza kufunga, akafunga mara tatu katika mechi ya ligi dhdi ya Racing Santander, na baadae akaja kuwaadhibu Real Sociedad. Hat trick yake nyingine ilikuwa katika mchezo wa fainali ya Europa League dhidiya Bilbao.


I - Inzaghi
Mara nyingi anapozungumzia wanasoka ambao wamemfanya awe alivyo sasa Falcao amekuwa akimtaja mshambuliaji wa zamani wa Azzuri na AC Milan Filliipo Inzaghi kama ndio mtu aliyekuwa akimsikuma mpaka kuweza kufikia hapa alipo leo.

J - Journalism
Wakati Falcao akicheza soka nchini Argentina, alijiunga na chuo kikuu cha Buenos Aires na akachukua kozi ya Journalism(Uandishi wa habari). Anasema ana mapenzi makubwa na uandishi na kila mara anapoulizwa kama asingekuwa mcheza soka basi sasa hivi angekuwa mwandishi wa habari.

K- Killer Instict
Falcao ana uwezo wa kutabiri wapi utadondoka katika eneo la penati la adui. Hisia  zake katika box la penati la adui zinamuongoza katika kufunga mabao mengi - ni hiyo ni moja ya sifa zake kubwa.

L - Leader
Sio kwamba Falcao ni kiongozi uwanjani , lakini nje ya dimba ni kiongozi wa kundi la vijana katika kanisa liitwalo Locos por Jesus.

M -Mop-top
Staili ya nywele ya Falcao ni gumzo katika kiwango dimbani. Nywele zake ndefu ambazo mara zote huwa anazifunga na mpira - imekuwa ni staili maarufu nchini kwao na imemfanya atambulike kiurahisi kuliko wachezaji wengine kwa mashabiki.

N - Nimble
Sifa nyingine ya Falcao uwanjani ni uwezo wake kuwa mwenye haraka na mwepesi awepo uwanjani.

0 - Opportunist
Falcao ana kawaida ya kuwa kwenye sehemu sahihi kwa muda sahihi na kufunga mabao muhimu katika nyakati muhimu. Hijalishi kama inakuwa tu ni bahati au uwezo, Falcao siku zote amekuwa akijua namna ya kuzitumia nafasi pale mpinzani wake anapofanya makosa.

P - Porto
Falcao alikamilisha uhamisho wake kwenda Porto kipindi cha kiangazi mwakak 2009, katika dili lenye thamani ya €4m. Kwa haraka akaonyesha uwezo wake, akifunga mabao 4 katika mechi zake nne za mwanzo. Mpaka anaondoka kwenye klabu hiyo alikuwa amefunga mabao 72 katika mechi 87.


Q - Quick
Sio kwamba tu Falcao huwa anawashangaza watu kwa nguvu na kuweza kufanya vitu kwa haraka na wepesi, lakini pia ana sifa nyingine - kasi. Kasi ambayo anaweza akapambana na mchezaji yoyote katika kuukimbiza mpira.

R- River Plate
River Plate ndio mahala alipoanzia soka la ukweli Falcao. Akiwa na miaka 15 alijiunga na academy ya klabu hiyo na akajichongea njia kwenda kucheza kwenye timu ya wakubwa. Akiwa na miaka 19, Falcao alicheza mechi yake ya kwanza na akaenda kufunga mabao 7 katika mechi 7 za kwanza. Pamoja na kuandamwa na majeruhi, mshambuliaji huyo alifunga mabao 49 katika mechi 110.

S - Speculation
Tnagu El Tigre Falcao aibuke kwenye ulimwengu wa soka, tetesi juu ya klabu kubwa zenye fedha kumtaka hasa kutoka kwenye premier league zimekuwa jambo la kawaida. Kwanza ilikuwa ni Spurs ambao walihusishwa na kutaka kumleta England, lakini zaidi hivi sasa ni Chelsea na City. Huku akiongeza idadi yake ya magoli kila siku ndivyo thamani yake inavyopanda, na kwa jinsi jina lake linavyoendelea kuwepo katika listi ya ufungaji kwa klabu na nchi yake, ninajiuliza kama kuna timu itaweza kulipa fedha ambayo Atletico wataitaka ili kumuachia.

T - Technique
Ufundi alionao huyo kiumbe unaweza ukachukua pumzi zako kwa sekunde kadhaa. Ana first touch nzuri sana, najua kuumiliki mpira na ni hatari sana katika kufunga haijalishi ni umbali wa 40 yards au 4 kutoka kwenye goli.

U- UEFA
Falcao alivunja rekodi ya magoli yaliyofungwa kwenye mchezo msimu mmoja wa michuano ya UEFA, ambapo alifunga mabao 17 katika michuano yote ya UEFA Champions League na Uefa League Cup katika msimu wa 2010-11.

V - Valuation
Ikiwa Falcao atafanikiwa  kuingia ndani ya Premier League, naotea kwamba klabu yoyote itakayokuwa na bahati itabidi itumie fedha nyingi sana. Falcao alienda Atletico kwa ada ya €40m kutoka Porto, na amefunga mabao 36 katika msimu wake wa kwanza. Kumekuwa na taarifa kwamba ikiwa klabu inataka kupata saini ya Mcolombia huyo, then itamgharimu kiasi cha €65m.

W - Winner
Katika kipindi cha miaka 7 aliyocheza soka la ushindani, Falcao tayari ameshashika makombe mawili ya Portuguese Super Cups, 2 Taca de Portuguese trophies, 2 Europa League, na moja la ligi ya Argentina na Uefa Super Cup.

X - X Factor
Falcao ana uwezo wa ziada, kitu cha ziada kinachomtofautisha na washambuliaji wengi. Ni vigumu kumuelezea na ukamaliza kwa kifupi tu Falcao ni mshambuliaji wa aina yake na anastahili sifa anazopata.

Y - Youthful
Pamoja na utajiri wake wa kipaji uwanjani, Mcolombia huyu anapendwa sana na wasichana na yote hii kutokana na kisura chake cha ujana, japokuwa anaelekea kutimiza miaka 27 siku chache zijazo.

Z - Zarate
Falcao ni jina kati la mshambuliaji huyo. Jina lake kamili ni Radamel Falcao Garcia Zarate
 

No comments:

Post a Comment