Search This Blog
Tuesday, September 18, 2012
HOJA YA MDAU Pascal Mwanjabala: Vodacom na TFF wanaipeleka wapi ligi kuu?
Ktk mechi ya Simba vs African Lyon,tImu ya African Lyon ililazimishwa kuvua jezi zao zenye nembo ya Zantel ambao ni wadhamini wao,na pia mabango ya Zantel yaliyowekwa Uwanjani yalitolewa,kisa nini?eti kwa kuwa tu Zantel ni washindani wa kibiashara wa Vodacom ambao ndio wadhamini wa Ligi Kuu bara(japo mpaka leo sijashuhudia wawakilishi wa klabu wakisaini huo mkataba),maswali niliyojiuliza ni haya
1.Kilio kikubwa cha klabu nchini ni kukosa udhamini nje ya ule wa Mdhamini wa Ligi Kuu,leo hii timu inapata mdhamini hafu anadhalilishwa vile,ni picha gani inajengwa kwa wadhamini wengine wenye nia ya kudhamini klabu zingine?
2. Udhamini wa Taifa Stars kwa mwaka ni sh.3.6bil kwa mwaka na Taifa Stars ina mechi zisizozidi 8 kwa mwaka, Udhamini wa Vodacom ni sh.1.3bil kwa mwaka na Ligi Kuu ya Bara ikishirikisha timu 14 inakuwa na jumla ya mechi 182 msimu mzima,kwa mazingira haya mdhamini huyu anastahili kuwa na exclusive right(haki ya kuzuia washindani wa kibiashara kudhamini klabu yoyote)
3.Ligi kuu ya Ghana inadhaminiwa na kampuni ya simu ya Glo,na klabu ya Hearts of Oak inadhaminiwa na kampuni ya simu ya MTN na huwa wanavaa jezi zenye nembo ya MTN,ukiachana na hao Ligi Kuu ya Uingereza inadhaminiwa na Benki ya Barclays na Klabu ya Liverpool inadhaminiwa na benki ya Standard Chartered ambao ni washindani wa kibiashara wa mdhamini mkuu na hamna mgogoro wowote....sasa hii jeuri ya Vodacom kutaka exclusive right inawatoka wapi tena wakisaidiwa na TFF?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
wangefanya simba azam au yanga wangewazuia? Au xana wangetaka upatanishi? Yanga hakuvaa logo zk match ngap na akamridhia na akamckiliza anachotaka?
ReplyDeleteJamani wenzetu walikuwa bize na issue za mbuyu twite na Yondani. tusiwasakame.
ReplyDeleteInategemea kwenye mkataba wa TFF, Vodacoma na vilabu vyote 14 walikubalina nini. Mambo yanayofanyika EPL na Ghana yako hivyo kutokana na mkataba wao wenyewe. Siyo "hard and fast rule" kwamba yanayofanyika EPL au Ghana lazima yafanyike huku pia.
ReplyDeleteHivi ligi ya bara inacmamiwa na kamati r TFF??me nafikiri pia yule mwenyekit wa kamati ni mamluki wa TFF na cdhani km kuna maana ya kusema ligi imedalisha usimamizi ila wanatuzuga tu!!
ReplyDelete