Search This Blog

Saturday, September 29, 2012

KWANINI CRISTIANO RONALDO NI TIGER WOODS WA SOKA

Cristiano Ronaldo ni mmoja ya wachezaji bora kabisa wa juu katika kizazi hiki. Jinsi alivyoitawala La Liga katika misimu miwili inatukumbusha mmoja wa wanamichezo bora kabisa katika karne hiii: Tiger Woods.

Pamoja na kwamba wanacheza kwenye michezo miwili tofauti, wawili hawa wana vitu vingi wanavyofanana. Wote wawili ni wachezaji muhimu sana katika michezo yao na wamaekuwa ni wenye mafanikio. Wameweza kupata madili mengi ya udhamini na huku wakicheza kwenye kiwango cha kuvunja rekodi.


Tiger na CR7 wamejituma sana mpaka kufikia malengo yao: wakicheza kwa kiwango cha juu ili kuwa wachezaji bora kabisa kwenye michezo yao husika.

Wawili hawa wanafanana katika vitu na hivi vifuatavyo ni baadhi.

MAPATO

Kwa mujibu wa Forbes, Tiger Woods ni mwanamichezo wa tatu anayelipwa vizuri zaidi duniani. Mshahara pekee unafikia kiasi cha $4.4 million kwa mwaka.

Cristiano Ronaldo pia yupo katika listi hiyo, akishika nafasi ya 9. Ingawa David Beckham anaongoza kwa mapato ya jumla, lakini mshahara wa Cristiano Ronaldo kwa mwaka upo karibia na $20.5 million, jambo ambalo linamaanisha anamzidi $11.5 million Beckham.

Hii inawafanya kuwa wanamichezo wenye kulipwa vizuri zaidi kwenye michezo yao - bila kuingiza mapato ya udhamini.

KUPENDWA NA KUCHUKIWA
Wanamichezo hawa wawili wana fan base kubwa sana na pia wanachukia sana. Kwa Tiger mambo yote yalianza ilipotoka skendo yake ya kumsaliti mkewe mwaka 2009. Taswira yake ya kuwa mume bora ikafutika na kuchukiwa na watu wengi.

Cristiano yeye na mwenzake Lionel Messi wamewagawa wapenzi wa mpira wa miguu duniani. Pia tabia zake za nje ya uwanja zimezidi kumuongezea maadui, muda mwingine tambo zake tu zimekuwa zikimfanya watu wamchukie.

Kwa wale wanaowapenda hakuna kitu kingine wanachojali zaidi ya ushujaa wao.

KIWANGO
Tiger ni mmoja kati ya wacheza gofu bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Wengi wanamuona kama ni bora zaidi ya Jack Nickalus, wengine wanaamini kwamba hatoweza kumshinda Jack mpaka pale atakaposhinda makombe makubwa zaidi ya 18.

Cristiano amekuwa nae akihusishwa na mjadala kama huo, lakini kwa mara nyingi zaidi amekuwa akifananishwa na Lionel Messi. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia na amekuwa akiendelea kutisha tangu wakati huo.

Wote wamekuwa kwenye viwango vya juu kwa miaka mingi, kwa Woods kipindi chake kizuri kabisa kilikuwa mwaka 2000.

Alishinda makombe sita mfululizo, kitu ambacho hakuna yoyote aliyeweza tangu mwaka 1948, alishinda katika michuano ya US Open,, kitu ambacho Sports Illustrated walisema kiwango cha Woods kwenye michuano hiyo kilikuwa bora kuliko vyote katika historia ya gofu.

Katika misimu 16 kama mcheza gofu, Tiger ameshinda katika michuano 102, 74 kati ya hiyo ameshinda katika PGA Tour.

Ronaldo amekuwa akicheza soka la ushindani wa juu kwa miaka 10 sasa ambayo amefanikiwa kufunga mabao 275 na Sporting Lisbon, Manchester United na Real Madrid, na mabao mengine 37 katika timu ya taifa ya Ureno, jumla ya mabao yote ni 312.

CR7 aliwakusanya mashabiki 85,000 katika utambulishwaji wake pale Bernabeu, akivunja rekodi ya Maradona ya kutambulishwa mbele ya mashabiki 75,000 alipoiunga na Napoli.

Alihitaji mechi nne kuweka historia na Los Blancos, alifunga katika kila mechi zake nne za mwanzo, akiwa ndio mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Moja ya mafanikio yake makubwa hivi karibuni aliweza kumaliza msimu wa La liga akiwa amefunga mabao 40, kitu ambacho hakuna aliyewahi kufanya hivyo; Hugo Sanchez na Telmo Zarra walikuwa wamefunga mabao 38 kila mmoja huko nyuma.

MITANDAO YA KIJAMII
Tiger Woods ndi mcheza gofu mwenye mashabiki wengi kwenye mtandao wa Twitter.

Alipofungua akaunti yake akuwa akitweet sana, lakini baada ya skendo ya kuisaliti ndoa yake, akaanza kuitumia akaunti yake.

Cristiano Ronaldo nae ana sifa hiyo hiyo ya Woods, lakini pia ameweza kuwa mwanamichezo mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mtandao huo akiwa na followers zaidi ya millioni 13.

MIKATABA YA UDHAMINI
Nike, NetJets, EA Sports, Konami, Rolex, na wengine kibao. Wote wanawadhamini hawa vijana. Wachezaji hawa wawili hawa wana wadhamini bora kabisa kwenye michezo.

Woods anatengezea kiasi cha $55 million kwa mwaka kutokana na mapato ya mikataba ya matangazo. Mchezaji huyo bora namba 1 wa zamani aliwapoteza wadhamini kama Gatorade, AT&T, Buick na Tag Heur katika miaka kadhaa iliyopita, lakini ndio mwanamichezo anayeokea fedha nyingi kutoka mikataba ya matangazo.

Katika upande wa Ronaldo anashika nafasi ya 10 na wa pili nyuma ya David Beckham kama mwanasoka mwenye mapato makubwa kutokana na mikataba ya matangazo ya biashara.

No comments:

Post a Comment