Search This Blog

Wednesday, September 26, 2012

ALEX SONG: USAJILI MWINGINE MBOVU KWA BARCELONA - MVIVU, MZITO NA ANAYEPEWA SIFA ASIZOSTAHILI


Ukiwa ni mwanachama wa klabu ya Alex Song, inabidi uachane na mpango wa kuendelea kuisoma makala hii kwa sababu takribani maneno 700 yanayofuatia hayatokufurahisha. Ikiwa wewe ni shabiki wa Arsenal, tafadhali endelea kusoma.

Kipande cha kwanza hapo juu kinaweza kikaleta kutokueleweka kwa sababu miaka kadhaa iliyopita, Song amekuja kuwa mmoja ya wachezaji waliopendwa na mashabiki pale Emirates. Alipendwa zaidi kiasi kwamba msimu wa 2011-2012 alipigiwa kura nyingi nyuma ya Robin van Persie katika tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Arsenal - kura zinazopigwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Mtandao wa Arsenal.com ulitoa hongera kwa Song: "Kwa miaka sasa, Alex amekuwa ndio msingi wa safu ya kiungo ya Arsenal, akitoa msaada mkubwa katika kuilinda safu ya ulinzi kutoka kwenye mashambulizi ya timu pinzani."
Wakati ikieleweka kwamba tovuti za vilabu mara nyingi zinakuwa zenye kutoa taarifa nzuri za wachezaji wao, lakini hili ni tofauti kwa upande mwingine. Ukweli ni kwamba Alex Song hana sifa anazopewa hasa katika kuilinda safu ya ulinzi. Katika misimu minne iliyopita, Arsenal wameruhusu mabao 170 ya kwenye ligi kuu tu. Katika kila msimu kati ya hiyo minne (kasoro 2009-10 wakati Spurs nao waliporuhusu kiasi sawa cha mabao), Arsenal wameruhusu mabao mengi kuliko timu yoyote katika Top 4 ya Premier League.

Sababu kuu juu ya suala hili sio udhaifu wa ukuta watu watano nyuma au mbinu mbovu za Wenger - au hata kama hizo nazo ni sababu lakini kubwa zaidi ni kwamba Song alishindwa kuilinda safu ya ulinzi.

Katika soka la kisasa ambapo unaweza ukawa na utegemezi kwa mabeki wa kiwango cha dunia, kui-control na kuiwezesha safu ya kiungo ndio mfumo mzuri wa ulinzi. Hii ndio maana timu zenye safu ya ulinzi ya kawaida zimeendelea kufanikiwa. Mfano mzuri ni safari ya Uholanzi mpaka kufika fainali ya World Cup 2010, ambapo Mark van Bommel na Nigel de Jong waliunda safu nzuri ya kiungo cha ulinzi kuwalinda akina Van der Wiel, Heitinga, Mathijsen na Van Bronckhorst. Song hawezi kuulinda ukuta wake kama ambavyo Van Bommel alivyokuwa akifanya. 

Song hana nidhamu ya kimchezo kiasi kuweza kupewa jukumu la mlinzi wa ngome ya timu. Wakati wachezaji wenzie wanapokuwa na kwenye kumiliki mpira, anashindwa kujizuia kujiunga na safu ya mashambulizi - hivyo mwishowe anaiacha nafasi yake na kuacha uwazi kwa wapinzani kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza. Wakati wapinzani wanapokuwa na mpira, uwezo wake kujitambua katika kujipanga na kuusoma mchezo ni dhaifu sana. Hizi mbinu ambazo huwezi kufundishwa, aidha uwe nazo au hauna. Spidi ndogo ya Song inamzuia kutoka kwenye kurudi kutoa ulinzi kwenye safu ya ulinzi mara anapoenda kushambulia. 

Kuna michezo mingi ya kuangalia jinsi Arsenal walivyodhuriwa kutokana na kuachwa kwa mashimo mengi kwenye mipaka ya ulinzi wa Song. Mchezo ambao ulionyesha vizuri udhaifu wa Song hivi karibuni kabla hajaondoka ulikuwa kwenye ligi ya mabingwa ulaya walipofungwa 4-0 na AC Milan.

Mashabiki wa Arsenal wanaimba nyimbo za kusifia assists 14 za msimu uliopita zilizotolewa na Song kama kigezo cha ubora wake, lakini kazi kuu ya kiungo huyo pale Arsenal ilikuwa ni kulinda magoli yasiingie kwenye lango lao na sio kuyatengeneza magoli. Rogerio Ceni amefunga mabao zaidi ya 100 pale Sao Paulo, lakini hilo halimfanyi kuwa golikipa bora.

Usajili wa Song kwenda Barcelona ni wa kushangaza. Ni usajili ambao sio makini kwa staili na filosofia ya uchezaji wa Blaugrana. Sio tu kwamba Song sio mwepesi tu pia ni mzito katika kukaba wapinzani, mara nyingi amekuwa akituhumiwa kuwa mvivu pia. Hii haitavumiliwa pale Catalunya ikiwa anataka kufanikiwa.

Kijana huyo mwenye miaka 24 hafanyi movements za haraka akiwa na mpira na hivyo yupo kinyume na staili ya Barca kumiliki mpira na kupiga pasi za haraka haraka na kuupeleka mchezo kwenye goli la wapinzani. Wakati Song ni mzuri ana katika kupiga pasi kuliko Mascherano, kuna wasiwasi kwamba kama ilivyotokea kwa Muargentina, Song nae atapata wakati mgumu kuweza kuendana na pasi za haraka, fupi na za pembe tatu na wenzie akina Xavi, Iniesta, Busquets, Messi na wengine.

Mascherano alihamishwa kwenda safu ya ulinzi katika jaribio la kuwa mbadala wa wa nahodha wao anayeandamwa na majeruhi Carles Puyol - na tangu wakati huo hajaangalia nyuma. Kuna uwezekano mkubwa Song nae anaweza akawa anatumika kwenye safu ya ulinzi, lakini hili litakuwa sio jambo zuri hasa kwenye mechi kubwa kama dhidi ya Madrid, Bayern au Man City. Katika mechi zake ambazo aliwahi kucheza nyuma Song alicheza hovyo, akionekana kukosa kujiamini.

Song ameanza career yake Barcelona akitumia muda mwingi kwenye benchi na hili linaonekana litaendelea, lakini €19 millioni ni fedha nyingi kutumiwa kwa mtu ambaye humtumii ipasavyo, na Tito Vilanova - ambaye mwenyewe aliomba Song asajiliwe anajiweka katika nafasi ya kuanza kulaumiwa.

Wakati aliyemtangulia Vilanova, Pep Guardiola alifanya usajili  mbovu wa wachezaji kadhaa - Dmytro Chygynskiy kwa ada ya €25m ndio uliotia fora - ni vigumu kuamini Guardiola angeweza kufanya usajili usio na tija kama huu wa Song - mchezaji anayepewa sifa asizostahili. Sio kwa mara ya kwanza katika masuala ya uhamisho kati ya Barcelona na Arsenal, lakini kwa mara ya kwanza ni upande wa Waingereza wamepata faida kubwa safari hii.

1 comment:

  1. wewe shaffih ndo mbovu...wote ni mashahidi ule ukuta wa barca ulivo kua weak ukilinganisha na safu ya kiungo na ushambulizi, lakini kwenye mechi hzi mbili tatu alizocheza song tumeona mabadiliko...angalio kuna uhai umeongezeka kidogo anapocheza song...so anaweza kuwa mbovu ukilinganisha na watu flan lakini pale barca kaongeza impact nzuri tu.

    ReplyDelete