Search This Blog

Tuesday, September 18, 2012

ADEBAYOR KUWANUNULIA JEZI MPYA MASHABIKI WA SPURS WALIONUNUA JEZI ZENYE JINA LAKE

Emmanuel Adebayor amefanya kitendo cha kiungwana kwa kuamua kumrudishia shabiki yoyote fedha alizonunulia jezi yake ya timu Tottenham yenye namba 25 mgongoni - jezi ambazo zilitangazwa na kuwekwa sokoni na Spurs kwa ajili ya msimu wa 2012/13 kabla ya mshambuliaji huyo hajaamua kubadili namba ya jezi na kuichukua namba 10 iliyokuwa wazi.

Adebayor aliuambia mtandao wa Tottenham:

"Namba 10 ni namba maalum kwanguna hivyo ilivyokuwa haina mtu nikaomba kama naweza kubadilishiwa namba ya jezi na klabu ikawa haina pingamizi juu ya hilo.

"Lakini walikuwa na wasiwasi juu ya jezi ambayo walishaiweka sokoni na mashabiki wakawa tayari wameshanunua ikiwa imeshandikwa jina la namba 25 tayari kwa msimu mpya.

"Ninajisikia furaha sana kwa kuwa mashabiki wa Spurs wanataka kuvaa jezi yenye namba na jina langu na sikutaka waathiriwe na mabadiliko niliyoyataka. Hivyo, nina furaha kubeba gharama za kuwawezesha mashabiki wote walionunua jezi mara kwanza kubadilisha kutoka Adebayor 25 - kwenda Adebayor 10.

No comments:

Post a Comment