Search This Blog

Sunday, August 12, 2012

MBUYI TWITE ATUA RASMI YANGA ATIA SAINI MKATABA


Mlinzi wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite amekalisha usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa kimataifa ITC na kuweza kujiunga na mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu ya Young Africans Sports Club.

Mbuyu Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya Lumpopo st.

Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Kagame.

Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'

"Unajua usajili sio mchezaji kusajuli makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.

Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya Young Africans kuwa na ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani, Nadir Haroub Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa katikati.

Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuaanza sepetemba mosi. 


Source: http://www.youngafricans.co.tz

10 comments:

  1. Wapi majigambo ya Kamwaga tunaomba accoment hapa maana alikuwa na tambo nyingi sana mara sijui rage mara wamembadilishia line ya simu Bin Kleb asimpate haya sasa mzee wa kubwabwaja Kamwaga leta unafiki wako hapa.

    ReplyDelete
  2. Nje ya uwanja hili ni goli jingine la takribani mita 45 yanga wanaifunga tena simba! Kimsingi naona Yanga wako vizuri ktk kuzielewa na kuzitafsiri sheria za uhamisho wa wachezaji kuliko simba. Rage kubali kwamba kwa hili ulikurupuka kama Kaburu alivyofanya kwa Yondani,. Simba mujifunze!!!

    Mbunge-Dom

    ReplyDelete
  3. Shaffih wewe simba tuu tukitoa comments zetu huweki au huu mtandao ni wa simba nini weka wazi sio kutubania.

    ReplyDelete
  4. Dah,hawa jamaa kiboko.kama namuona mr.liverpool akipost FaceBook,nipo na bamutu ba simba tunakunywa kahwa,alafu akapost yanga yapigwa bao la 3,baada ya ngassa,okwi sasa bao la 3.Nilimwambia yanga hawakumtaka ngassa,wangemtaka simba hasingetia mguu,mzee mzima Rage katoa chozi,vijana wabaya hawa

    ReplyDelete
  5. Du kuwahi baa siyo kulewa wahenga walisema,hivyo ,hapa simba watulie mtu mzima usipokuwa makini kwa hili unaweza kuzirai.AWADH -MVOMERO MORO

    ReplyDelete
  6. mwisho wa yote haya ligi itaanza tutawaona huyo twitte.perfomance yake hapa tutachekana.......yanga mikwara mingi ila hamna good future na wachezaji coz kwa takwimu hamjauza mchezaji nje ya africa kwa zaidi ya miongo 3 ukumuachilia nonda shabani sasa mi sidhani jama mbwembwe za kusajili ni bora kuliko ushiriki ktk ligi ya ndani na africa

    ReplyDelete
  7. hiyo ndo bongo na michezo bwana

    ReplyDelete
  8. Viongozi wa yanga sio kiboko ni wapuumbavu rudisheni pesa ya Simba mbaki na twite. Wenu na magoli mtapigwa. Wako. James

    ReplyDelete
  9. I don`t think that Yanga peoples are clever, because what they have done is nothing in soccer development generally in Tanzania. There are alot of prayers how do they stand to do the rubbish things like that.

    at the end of the day, home groud , away out!!!!!!!!!!!!

    Leaders are not focus ahead.

    Rubbish!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete