Search This Blog

Thursday, July 12, 2012

Yanga yatangaza kikosi cha Kagame

ZIKIWA zimesalia siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Kagame kuanza, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji, Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaocheza huku akimtema nahodha wake, Shadrack Nsajigwa .

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi, keshokutwa Jumamosi na siku hiyo itafungua kwa kuanza kucheza na Atletico ya Burundi.

Akitangaza kikosi hicho, Tom alisema haikuwa kazi rahisi kwake kupata kikosi hicho kutokana na viwango vya wachezaji wake kwenye tim hiyo.

Saintdiet alisema, wachezaji ambao amewaacha wasisikitike akiwemo Nsajigwa anatambua umuhimu kwenye timu na badala yake waendelee na mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbelgiji huyo amekitaja kikosi hicho kuwa ni makipa ni Yaw Berko na Ally Mustapha ‘Bartherz’, Mabeki ni Juma Abdul, Godfrey Taita, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani  ‘Vidic’, Ladislaus Mbogo.

Viungo ni Athumani Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Rashidi Gumbo, Nizar Khalfani, Shamte Ally na Idrisa Rashidi

Washambuliaji ni Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi na wachezaji aliowaacha ni Stephene Mwasyika, Ibrahim Job, Said Mohamed, Nsajigwa Omega Seme, Frank Domayo na Simon Msuva waliopo Timu ya taifa ya vijana ya U-20, Nurdin Bakari mwenye majeraha ya paja.

4 comments:

  1. KWA KIKOSI HIKI MKITETEA UBINGWA SIJUI.

    ReplyDelete
  2. I am respecting the selection done by the coach, but I am not comfortable with the exclusion of Stephano Mwasyika,for me this is the best left defender in the country.Best wishes. By Mwl.Malele,Shikula S.S.(Mbozi).

    ReplyDelete
  3. Wewe mwalim Malele huyo Mwasika hana lolote au unapenda wachezaji wanaopiga marefa?? Kila tukiingia Taifa SImba wanaimba Huu Haaa kwa ajili ya huyo Mwasika na fiatu fyake

    ReplyDelete
  4. Kikosi kizuri mwalimu kaangalia uwezo na sio majina tuta tetea ubingwa wetu.

    ReplyDelete