KLABU YA TSG HOFFENHEIM YAIALIKA TSC MWANZA KUFANYA NAO MAZOEZI - WALA CHAKULA CHA USIKU PAMOJA
Wakiendelea na ziara yao nchini Ujerumani - timu ya TSC Mwanza leo imealikwa na kufanya mazoezi ya pamoja na kubadilishana mbinu mbalimbali na klabu ya TSG 1899 Hoffenheim under 19 ya Ujerumani. Klabu zilianza mazoezi jioni na baada ya kumaliza walikwenda kujisafisha kabla ya kupata dinner ya pamoja.
Dauda nilikuwepo
Nikiwa na wachezaji wa TSG Hoffenheim na TSC Mwanza baada ya mazoezi
Mazoezi ya pamoja
Kocha wa TSC Mwanza Bwana Kaijage alipewa zawadi ya jezi ya klabu ya TSG Hoffenheim
BAADA YA MAZOEZI NAHODHA WA TIMU TSG HOFFENHEIM ALITOA RISALA YA KUWASHUKURU TSC MWANZA
MENGINE YAKAENDELEA
KATIKA PITA PITA YANGU KWENYE JENGO LA TSG HOFFENHEIM - NIKAINGIA KWENYE LAUNDRY
HAPA NI GYM YA ACADEMY YA TSG HOFFENHEIM
WABONGO TUIGE HII KITU - PROGRAM NZIMA YA MAZOEZI NDANI YA MWEZI
BAADA YA YOTE - HATIMAYE VIJANA WAKAKARIBISHWA DINNER
Kweli bado tuko mbali sana; ila tatizo letu ni kuwa hizi klabu kubwa Simba na Yanga zina mtaji wa kutosha kufanya haya ila wajanja wachache wanatuangusha. Napenda niwalaumu watu wa Media kama ninyi akina Shaffii kwa kuendelea kuwapamba hawa viongozi kama akina Kaburu, Rage, Malinzi ambao kwa ufuatiliaji wangu ni waganga njaa zaidi na wala hawana utashi wa kweli kusaidia soka la Tanzania.

ReplyDeleteNdugu yangu shafii tafuta basi camera nzuri urekodi clips ndefu kidogo unatuboa na vipande vifupi fupi unavyotuwekea
ReplyDelete