Search This Blog

Friday, July 27, 2012

CRISTIANO RONALDO, DROGBA, ETO'O NA WACHEZAJI WENGINE SITA AMBAO ILIBAKI KIDOGO WASAJILIWE NA ARSENAL


Huku taarifa za kusajiliwa kwa Yann M'Villa zilipokuwa zimepamba moto siku chache kabla ya Euro 2012, kila aliamini kinda hilo la kifaransa litakuwa ndio usajili wa pili Arsene Wenger baada ya Lukas Podolski. Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti Arsenal hawana mpango wa kumsajili tena M'Vila. Hili sio jambo geni kwenye soka na sio geni kwenye klabu ya Arsenal hasa kwenye kipindi hiki cha uongozi wa Arsene Wenger.

Hawa hapa ni wachezaji wengine ambao Wenger alikaribia kuwasaini akiwa Arsenal.


ZLATAN IBRAHIMOVIC
Akiwa na miaka 19, Zlatan alikuwa amekaribia kabisa kujiunga na Arsenal kutoka Malmo kwa ada ya uhamisho wa £3million mwaka 2000, hapo ilikuwa hivyo mpaka Wenger alimpotaka mchezaji afanye trial-majaribio kabla ya kusajiliwa rasmi. Lakini kwa Zlatan hiyo akaona ni dharau akaamua kuachana na Arsenal ambao tayari walishampa jezi.

JUAN MATA
Wakati wa kiangazi mwaka 2011, ambapo mtoto wa Catalunya Cesc Fabregas alipokuwa akililia kurudi nyumbani Nou Camp - na ikaonekana na dhahiri anaondoka Arsenal walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Juan Mta kusaidia kuziba pengo la Cesc. Huku wakiwa na fungu la kutosha walilolipwa na Barca wakaanza kujichelewesha ili kuishinikiza Valencia imuuze kwa bei chee mchezaji wao, Chelsea wakaingilia kati na kutoa kisu kilichohitajika na wakafanikiwa kumsajili kwa ada ya £24 million

PETR CECH
Baada ya kumtongoza kwa muda mrefu, ilionekana kama Cech alikuwa anajiunga na Arsenal akitokea Sparta Prague mwaka 2002. Timu zote zilishakubalina bei na mahitaji binafsi ya mchezaji lakini kibali cha kufanyia kazi kikawa kikwazo kikaleta shida na Arsenal wakaona waachane na mpango wa kumsajili, badala yake akajiunga na timu ya Ufaransa Rennes kabla ya baadae kwenda kujiunga na klabu ambayo imemfanya kuwa moja ya magolikipa bora duniani. Chelsea.

DIDIER DROGBA
Wenger aliwahi kufunguka kwamba alikuwa na nafasi ya kumsajili Drogba kwa pesa ndogo isiyozidi hata mshahara wa wiki wa mchezaji wa Chelsea (£100,00)

" Tulikuwa tunamuangalia vizuri Drogba lakini tulihisi hakuwa tayari kucheza England," Wenger alisema, "Lilikuwa ni kosa kumkosa Didier lakini unapokuwa kwenye soka, kila mtu anaweza kuelewa. Hata hivyo tayari tulikuwa na Thierry Henry."


SAMUEL ETO'O
Akiwa ndio anaondoka Real Mallorca kama mfungaji wao bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya La Liga akiwa amecheza misimu mitatu tu, Eto'o alipewa ofa kujiunga na Arsenal in 2004 na Wenger, ingawa mshambuliaji huyo na tabia yake ya kujisikia ilimfanya kocha wa Arsenal ajiulize mara mbili mbili amsajili au la mchezaji ambaye hivi karibuni alisema kumtandka wakala wake ilikuwa ni idea nzuri. Arsenal hatimaye wakajitoa kwenye mbio za kumsajili mcameroon ambaye nae alsema chaguo lake lilikuwa ni Barcelona.

CLAUDIO MAKELELE
Mwaka 1996 Wenger alikamilisha usajili wa kiungo Patrick Vieira kuja Arsenal. Wiki moja baadae akapokea simu kutoka Nantes ikimuuliza kama Wenger atakuwa tayari kumsajili kiungo Makelele.

Mazungumzo yakafanyika na dili la Makelele kuelekea London lilikuwa karibu (kwa mujibu wa mahojiano ya Wenger aliyoyafanya 2006) ingawa Wenger akajitoa kwenye bio za kumsajili kiungo huyo, akimtegemea Vieira.


YAYA TOURE
Huku kaka yake mkubwa Kolo akiwa ameshasajiliwa tayari, Arsenal walionekana kama wanataka kuuteka ukoo wote wa Toure, walimpotaka kumsajili Yaya. Alienda london na hata kufanikiwa kuichezea Arsenal ya vijana kwa mchezo mmoja kabla ya suala la vibali vya kazi kuleta tena utata na Toure akaenda kujiunga na Olympiakos kalba ya kuja kuwa mmoja ya viungo bora kabisa wa kati duniani akiwa na Barcelona na Man City.

CRISTIANO RONALDO
Stori ilikuwa hivi...... akiwa mdogo Ronaldo alionyeshwa jiji la London lilivyo na kupelekwa mpaka uwanja wa Arsenal na kupewa jezi la Gunners ikiwa na jina lake nyuma na Arsene Wenger mwenyewe.
Arsenal hawakuishia hapo walifiikia mpaka hatua ya kukubaliana ada ya uhamisho ya £4million na Sporting Lisbon.

Then, kwa bahati mbaya, Lisbon wakacheza na Machester United in 2003 kufungua uwanja wao mpya. Ronaldo akacheza mchezo huo na kuwapeleka puta sana United, na mwishowe Sporting wakashinda kwa 3-1. Wakiwa kwenye ndege kurudi England wachezaji wa Man U wakamshawishi Fergie amsajili CR7, na babu nae akatuma ofa ya £12million kisha kocha msaidizi wa United wakati huo, Carlos Queiroz akaenda kuongea na Ronaldo na wakala wake na akafanikisha dili hilo ambalo limeigharimu sana Arsenal.

No comments:

Post a Comment