Search This Blog

Monday, July 23, 2012

CANTONA ARUDIA KUPIGA KUNG FU - BAADA YA MANCHESTER UNITED KUKOSA UBINGWA WA EPL MSIMU ULIOPITA


Imefichuliwa kwamba Eric Cantona alikasirika mno kiasi cha kufikia kuipiga mateke meza ya kunywea kahawa baada ya kuona Manchester United wakipoteza ubingwa wa Premier League msimu uliopita.

Mwanae wa kiume Raphael alifichua bado ana mapenzi makubwa na United.

Alisema walikuwa wawili wakiangalia mechi za mwisho za ligi kuu ya England  na akawa na matumaini makubwa kwamba Manchester United watabeba kombe huku mahasimu wao City wakikamatwa na QPR.

Lakini Sergio Aguero akafunga goli la ushindi sekunde kadhaa kabla ya kipenga cha mwisho, na kuipa City ubingwa wa kwanza katika cha miaka 50 kwa tofauti ya magoli.

Cantona akiondolewa na mapolisi kwenye uzio wa uwanja baada ya kumtwanga shabiki wa Crystal Palace.

Raphael, 23, alisema baba yake, ambaye anakumbukwa sana kumpiga mateke ya kung fu shabiki wa Crystal Palace Matthew Simmons mwaka 1995,  alirudia kitendo chake lakini safari hii hakuwa binadamu aliyepigwa mateke bali ni meza wanayotumia kunywea kahawa.

Mtoto huyo wa kiume aliwaambia waandishi habari: "Aliivunja vunja ile meza. Baba alikasirika sana. Bado anaipenda sana United na tulikuwa tuna matumaini watabeba kombe jioni ile."

 

No comments:

Post a Comment