Baada ya jitihada kubwa ya kusaka goli la ugenini katika kipindi cha kwanza timu ya Taifa kwa soka la wanawake ya Ethiopia walifanikiwa kulipata dakika ya 69 na kuiondoa wanawake wenzao Watanzania 'Twiga Stars' kwa jumla ya goli 3-1.
Katika mchezo huo wa raundi ya mwisho kusaka tiketi ya kufuzu mataifa ya Afrika kwa Soka la Wanawake yatakayo fanyika hapo baadae nchini Gabon, uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa Ethiopia kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Katika mchezo huo, hususani katika kipindi cha kwanza ulibidi Twiga Stars wabaki nyuma wakiokoa hatari lukuki na shukrani zimuendee kipa wa Twiga Stars na safu nzima ya ulinzi kuzuia mashambulizi ya Ethiopia katika kipindi chote cha kwanza.
Baada ya jitihada za kuzuia mashambulizi ya Waethiopia, katika dakika 69 walinzi wa Twiga Stars walifanya kosa lililo wapa ushindi Ethiopia na kukata tiketi ya kwenda Gabon.
Katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Adis ababa ulimalizika kwa Twiga Stars kufungwa goli 2-1, hivyo kuondolewa kwa jumla ya goli 3-1.
No comments:
Post a Comment