Search This Blog

Thursday, June 21, 2012

TETESI HAI - NYUMBANI NI NYUMBANI: MRISHO NGASSA NJIANI KURUDI YANGA

Yanga wameendelea kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa.

Habari za ndani zinadai kwamba zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
"Leo saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.

Katika usajili huo Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa.

6 comments:

  1. Duuuh! Ya kweli hayo? Teh! Teh! Teh! TeeƩeeeeh!

    ReplyDelete
  2. Bora aeende Hata bure ametukosesha magoli kibao mechi za azam na yanga

    ReplyDelete
  3. Hv shaffih ww kwenye spotbar si ndo ulisema sajili za yanga ni magumash na ni kampen na kwamba mwisho wa siku ukwel wako utaonekana sasa sjui ulikua sahh au we ndo magumash

    ReplyDelete
  4. Haukumuelewa shaffih usajili wa tnzania nimagumashi ndio lakini hapa shaffih anatupasha habari za usajili sasa utajaza mwenyewe katika kung'amua
    SAFI SANA SHAFFIH AKA PELLE WA BONGO

    ReplyDelete
  5. Mimi siamini,akilini hainiingii kabisa huwezi ukambadilisha Nurdin Bakari na Mrisho Ngassa!! Nurdin Bakari ni kifaa adimu sana kwa hapa Jangwani. Yanga kuweni makini sana na uamuzi huo. Ngassa ni muhimu kurudi Yanga lakini sio sahihi kumuachia Nurdin Bakari arudi Yanga. Fanyeni kila liwezekanalo kuhakikisha Nurdin na Ngassa Wanakuwepo Jangwani.

    ReplyDelete