Search This Blog

Sunday, June 17, 2012

KWANINI WACHEZAJI WAKUBWA WALIOTAMBA BARANI ULAYA WANAKIMBILIA UARABUNI KUCHEZA SOKA?

Raul Gonzales akitambulishwa kujiunga klabu ya Al Sadd ya Qatar hivi karibuni.
Katika miaka ya hivi karibuni nchi za kiarabu haswa nchi ya Qatar ndio imekuwa ikionekana kuongoza mbio za kuwasajili makocha na wachezaji wenye makubwa waliotamba kwenye ramani ya dunia ya soka kupitia vilabu vyao tofauti.


Wachezaji wakubwa kama Gabriel Batistuta, Eric Djemba Djemba, Marcelly Desailly, Christopher Dugarry, Claudio Caniggia, Jay Jay Okocha, Taribo West, Frank and Ronald De Boer, John Utaka, Mario Basler, Hakan Yakin, Paulo Wanchope, Juninho Pernambucano,  Stefan Effenberg, Emile Mpenza, Youseff Chippo, Tony Yeaboah, Victor Ikpeba, Titi Camarra, Abedi Pele, Frank Lebouef, Pep Guardiola, Mauro Zarate(anayecheza Inter Milan) walishawahi kucheza soka nchini Qatar, Huku makocha wakubwa kama Bruno Metsu, Rene Meulesteen wa Man United, Bora Milutinovic, Emerson Leao, wakiwa tayari wameshafundisha soka ndani ya nchi hiyo kwenye miaka kadhaa iliyopita huku wengine wakiwepo na wakiendelea na kazi zao.

Pia wachezaji kama, Mamadou Niang, Kader Keita, Karim Zian, Mario Melchiot, Aruna Dindane, nahodha wa Korea Kusini Lee Jung-Soo bila kumsahau mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid na klabu bingwa ya ulaya  Raul Gonzales Blanco wamekuwa sura mpya za mastaa walioweka vizuri barani ulaya na Afrika kuwepo ndani ya soka la Qatar.


Qatar ambayo yenyewe tofauti na nchi zingine za kiarabu yenyewe miaka kadhaa ya nyuma haikuwa ikionekana sana kwenye ramani ya soka, leo hii ndio nchi ya kiarabu yenye mafanikio makubwa kuijumla ya kisoka ndani ya miaka miwili iliyopita, wakifanikiwa kuwashinda Waingereza na wamarekani kwenye mbio za kuandaa faianli ya kombe la dunia mwaka 2022, huku kubwa klabu ya nchi hiyo ikibeba kombe la mabingwa wa Asia mwaka jana.


Pia makampuni makubwa na matajiri wa nchi hiyo yamekuwa yakiwekeza sana kwenye soka, kwa mfano mwaka jana tulishuhudia klabu ya Barcelona ikivunja mwiko wa kutokuwa na mdhamini wa jezi baada ya kuingia mkataba mnono na Qatr Foundation, huku pia klabu ya Malaga ya Spain ikinunuliwa na tajiri raia wa Qatar, bila kuwasahau matajiri wapya wa ulaya klabu ya PSG inayomilikiwa Qatar Investment Authority.


Baadhi ya wadau wa soka ulimwenguni nikiwemo mimi nimekuwa nikijiuliza namna nchi hii sasa inavyojaribu kuuteka ulimwengu wa soka, na ndipo nilipokutana na mchezaji wa klabu ya Al Sadd Ally Hassan Afif nikafanikiwa kupata majibu yangu.


Afif anasema: "Baada ya muda mrefu nchi yetu ya Qatar kupigwa bao na majirani zetu kama Oman, Saudi Arabia na wengineo kwenye soka, ndipo serikali pamoja na wadau(vilabu) wa soka wa Qatar walipoamua kuwekeza kwenye soka na kuweka mipango bora itakayovutiwa wachezajiwa kigeni kuja kucheza hapa.
Kwanza katika kuifanya soka ya Qatar itambulike kimataifa wakanza kuwasajili wachezaji wenye umaarufu mkubwa huku wakiwa wanawalipa fedha nyingi bila kukatwa kodi, pia wakawa wanasaini makocha wenye ujuzi na majina kwenye ramani ya dunia ya soka.
Kupitia hili vilabu vilifanikiwa kuwavutia wachezaji wengi maarufu na wenye uwezo kujiunga navyo, kwa kuwa walikuwa wakilipwa fedha nyingi sana kama ilivyo barani ulaya lakini kwa Qatar wakiwa hawalipi kodi, kiukweli hili ndilo limesaidia sana kuitangaza nchi yetu, hivyo hii ndio siri kubwa inayowafanya wachezaji kama akina Raul wamekuja kucheza soka huku.
Jambo lingine ambalo lilikuwa kwenye mkakati ni kuweza kupata nafasi ya kushinda uenyeji wa kuandaa michuano ya kombe la dunia na alhamdulilah mwaka jana tulifanikiwa kwa hilo na mungu ankipenda mwaka 2022, Qatar tutacheza World Cup tukiwa kwenye ardhi yetu.
Pia serikali na wafanyabiashara wakubwa kupitia makampuni yao makubwa wakaanzisha mkakati wa kununua vilabu maarufu barani ulaya pamoja na kutoa udhamini, ndio tunavyoona Paris Saint-German na Malaga zote zimenunuliwa na watu wa Qatar, huku Barcelona ambayo ndio klabu ya pili kwa umaarufu duniani baada ya Manchester United, wakiwa wanadhaminiwa na Qatar Foundation. Hii siri ya mafanikio ya nchi ya Qatar katika kuendeleza soka letu pamoja na kufahamika kwenye ulimwengu wa soka."
 

No comments:

Post a Comment