Hi Mr. Shaffih, Jana usiku nilikuwa nasikiliza kipindi chenu cha Michezo Sports Extra na Sports Bar, vilivyorushwa kwa wakati mmoja kupitia Clouds Fm na Clouds Tv. Nilisikiliza kipande ambacho kuna Mzee Anayeitwa Akilimali, ambaye hujiita katibu wa Baraza la Wazee Wa Yanga. Sina uhakika na hiyo nafasi kwenye Katiba ya Yanga kama ipo.
Amekuwa akitumika sana, nashukuiru kwa kulitambuahilo jana. Waandishi mmempa sana airtime ya kutosha huyu Mzee mpaka imekuwa kero. Amekuwa Msemaji Mkuu wa Yanga kinyume na utaratibu. Wakati wachezaji wetu wamempiga refa Mechi ya Yanga na Azam alilumbana na TFF na kuongea mambo ya ajabu. Kwenye birthday ya Yanga aliwasifia akina Nchunga na akawageuka baadaye. Jana tu Anasema uchaguzi wa Yanga ukiisha atamfukuza Mwanachama Abedi Falcon uanachama kisa ameweka pingamizi kwa wagombea kuhusu uchaguzi.
Kwani hajui ni haki ya mwanachama kuweka pingamizi? alisema ana milioni 750 za usajili, azitoe wapi? Mzee yule na wenzake wasioitakia Yanga Mema ndio hao wamewaponza wachezaji wetu wa Yanga leo hii wamekosa fursa muhimu ya kutumikia timu ya Taifa kutokana na kuwatumia mechi zetu za mwisho wacheze maigizo ili kumkomoa Nchunga. Kiko Wapi leo? Menyekiti hayupo Yanga na Yanga itaendelea kuwepo. Timu yetu ilipoteza muelekeo mwishoni mwa ligi kwa hujuma za hao wazee dhidi ya Uongozi halali.
Leo wachezaji wanasajiliwa na watu binafsi kwa gharama kubwa, kwa akili ya kawaida wanayanga wanachekelea tu bila kutafakari. Mchezaji anasajiliwa kwa Milioni 30 na Mshahara M 1 kwa chanzo gani cha mapato klabuni? hao wanaowatumia akina Akilimali wakigombana na viongozi halali si ndio wanagoma kutoa mishahara, na kupigwa zile tano? tuna safari ndefu Kaka. Nahitimisha na kusema yule Mzeee alikuwa anatumika tangu mwanzo wa mgogoro wa Yanga, na ameendelea kuwa Msemaji Mkuu, Sekretarieti ya Yanga inamuchia, Nyie waandishi wa Michezo mnampa nafasi bila sababu. Ni bora mmemgundua. Mimi ni Mshabiki wa Yanga wa Kawaida, huyo Mzee hana Mamlaka ya kunivua ushabiki ndio maana nimefunguka.
Mr. Faraja Emmanuel Mkazi wa Kurasini.
0717 079727



Kiukweli sijawahi ona mzee anayetumikishwa kama huyu ati,we kweli kizee kama ichi hz m700 apate wapi kwanini asingetoa kipindi kile team inaukata akapunguza matatizo kuliko fikra zake za kijinga daily,na aliyempa jina la AKILIMALI ni mjinga,huyu alipaswa apewe AKILIMATOPE.
ReplyDeleteHatari ambayo watu hawaioni au hawaisemi ni kwamba Mzee huyu anazua hasira kwa wanachama kwa tuhuma ambazo hazina uthibitisho, matokeo yake watu watachukua sheria mkononi kwa kuamini maneno ya huyu mzee. Nilitegemea hata vyombo vinavyohusika na usalama kukemea tabia hii. Suala hili likifuatiliwa ni rahisi kuwabaini wanaomtumia kwa kuwa uongozi ukiondolewa kwa fitina kuna watu wanajitokeza harakaharaka, inabidi uchunguzi uanzie kwa hawa!!!
ReplyDeletenice word Faraja, heri yamemkuta Shaffih ili aanze kushirikiana na wenzake pale studio kuondoa huu upuuzi hasa wa huyu mzee. shabiki wa Yanga!
ReplyDeletekwani yanga inatumia senti ngapi yako?ss hao wanaosajili kwa kuikopesha yanga hata kama watakuja pata return kubwa,ww inakupunguzia senti ngapi yako?au ww namba yako ya uanachama ni ngapi?wacha kutuwiwa kinyume na m... Na huyo shaffih
ReplyDeleteshaffih,pole sana kwa kuingia kwenye malumbano na huyu mzee aliegeuka kua celebrety from no where,bt am sure ni nyinyi watu wa media mmemfikisha hapo na sasa kaota mapembe,ni kweli kua anatumika swala ni nani anamtumia na kwa maslahi yapi?wazee wa aina hii ndio wanalipeleka soka letu shimoni kwani anaishi kwa unafiki na migogoro kwake ndio shangwe,naomba klabu ziwe imara na kulinda katiba zao na kila kamati itekeleze majikumu yake sio mtu kujichukulia madaraka na kua msemaji na mtoa hukumu za kuhamasisha kuchukia watu na kuwafukuza uanachama ni hatari sana kuendesha soka kwa mtindo huu.Nakusihi umbane athibitishe kauli zake kwa vielelezo ili watu wajue unafiki wake na wasimuamini na uzandiki wake
ReplyDeletechela wa dom
nakushukuru kaka kwa maana umefunguka na umeweka uwazi wako kaka,mimi sitaki kukulaumu, ila nataka kukuambia umeangalia "tulipoangukia na sa sio tulipojikwaa", soka la bongo and YANGA in particular lina matatizo makubwa, nitajipanga kukupa baadhi ya mambo yanayotukabili YANGA.
ReplyDeleteYonah
Habari ya kazi Bwana Shaffih Dauda na wadau wote kwa ujumla wake, kwanza nimshukuru Mtoa mada Bwana Faraja Emmanuel kwa maelezo yake yakinifu kabisa, ameeleza mengi ambayo nilitaka kuyasema pia ila mimi bado nalia na waandishi wetu wa habari sina nia ya kuwavunjia heshima ila kusema ukweli waandishi wetu wa habari wa Tanzania wengi either hawajiamini,ama hawako qualified, ama nao wanatumiwa ama wameweka pembeni taalum zao wakaingiza ushabiki. Kwa nini na watuhumu?Mimi pia nilipata bahati ya kusikia maelezo aliyoyatoa Mzee Akilimali na kwa bahati nzuri na kwa kuonyesha kwamba unajiamini na huna hatia umeyaweka tena kwenye web yako, nimependa huo ujasiri.Turudi kwenye tuhumu nilizota juu ya waandishi wa habari hivi mtu anapoita Press Conference anakuja kutoa tuhuma nzito juu ya mwandishi mwenzenu tena anakuja bila hata vidhibitisho ama ushahidi na waandishi wa habari wanamsikiliza kisha wanaondoka kwenda kuripoti huo ni uandishi gani wa habari kwa nini waandishi walishindwa kumbana Mzee Akilimali atoe ushahidi hii ni karne ya sayansi na Teknolojia kama kuna Email, ama sms toka kwa Maximo akilalamika kwamba Shaffih anampigia simu na kumtumia Email na wanadai wanaushahidi kwanini asizi print akaja nazo kuonyesha wakati anatoa malalamiko yake ila waandishi wa habari kwa kuwa nao wanamuogopa mzee Akilimali wakacheka wakaogopa kumbana kwa maswali labda wakihofia kufukuzwa wakawahi kwenda kuripoti ili waonekane wanaipenda Yanga.
ReplyDeleteNaomba nimtaje mwandishi wa habari ambaye mimi aliwahi kunivutia sana huyu ni Maulid Kitenga nadhani wengi mtakumbuka kipindi cha uongozi wa MH: Ndolanga,huyu bwana Maulid alikuwa jasiri na aliweza kumuuliza maswali pasipo woga wowote na kumbana hadi kupata ukweli hii ilipelekea Ndolanga kuwahi kumtukana Kitenge ila mwisho wa siku kwa kuwa alikuwa anajiamini na alikuwa anaheshimu kazi yake alifanya na nakumbuka alichaguliwa kuwa Mwandishi bora si kwa kumbana Ndolanga hapana ila kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kwenda extra miles ili kudhibitisha ukweli na hakuwa mwoga.
Sitaki kusema sana nisije nikajaza huu ukurasa ila, waandishi wa habari wanatungusha waache woga ama nao wanalipwa kuripoti?.Sijui Shaffih mwenyewe ana msimamo gani juu ya tuhumu hizi ila kwa hali ya kawaida huyu mzee alipaswa kumsafisha juu ya tuhuma hizi, nasema hivyo kwa kuwa vilabu hivi vikubwa vina mashabiki wengi ambao si waelewa na wanatumika vibaya huwezi jua mtu anaweza kukufanyia kitu gani kisa tu yeye kwake mzee akilimali ni kama malaika ni lazima uwe makini.Nakumbuka Refaree mmoja aliwahi kupigwa jiwe baada ya mechi akazimia na alipigwa na mtu ambaye alikuwa anaonekana kama mwendawazimu kisha akakimbia na alimpiga na jiwe siku moja baada ya huyo mwamuzi kuchezesha mechi na timu ya mkoa huo ikafungwa nyumbani hiki ni kisa cha kweli japo kimetokea siku nyingi siwezi kumtaja Mwamuzi ila mwisho wa siku kumbe yule hakuwa chizi ila alipewa mkwanja akaambiwa avae kama chizi halafu amzibue.
Mwisho, Maximo is a professional Coach na ni mtu mzima mzee Akilimali anapaswa kufahamu hilo huwezi sema ameambiwa asije wakati mkataba anaingia na Yanga na si Bwana Dauda, mzee Akilimali aache uhuni na yeye si msemaji wa Yanga na hana mamlaka ya kumfukuza mtu uanachana, hao wazee wanajiona miungu watu wakati hawana lolote njaa tu.
Mdau
Mike.
Huyo mtoa mada ni feki, unaweza kuwa ni mwenyewe Shaff, wewe jamaa ni muongo sana na mtu wa majungu sana. Nimepiga hiyo namba, haipo. Kama una ugomvi na Yanga just come out and move on, siyo kipindi chake hiki.
ReplyDeleteMdau
Washington
shaffih umeweka makala hiyo unatuzuga tu ww mwenewe unatumika kila siku yanga yanga yanga mbon rage aliwadanganya simba anawajengea uwanja hujawahi kuhoji au kuweka habar hzo hapa acha kutumika shafiii
ReplyDeleteAkilimali hamjui ata shafii wakati kawaita wana habari kutoa malalamiko ebu tizama vizuri hiyo video anashindwa kumkumbuka jina mpaka asome inaonyesha kuna watu wamempa akayaseme, yanga imekuwa kama jalala..
ReplyDeletemtaniwia radhi mashabiki wa yanga ila nna wasiwasi na akili zenu, sidhani kama zimetimia. hivi kweli kabisa mtu unaweza kupoteza muda wako kwa kumtetea huyo mzee ambae ni marehemu mtarajiwa? lipi la maana ambalo amewahi kuongea katika muda wote aliowahi kuongea na vyombo vya habari? na kama huyo ndie anaetegemewa kuongea mambo ya yanga basi hao waliobaki nadhani ndio mazuzu kabisa. jamani hebu badilikeni hata kama kadi zenu zimeandikwa bishana ukishindwa pigana!
ReplyDeleteHuyo jamaa anijiita Washington inawezekana akawa anaulemavu wa akili asidhani kubahatika kujuwa computer na kuweza kufungua blogs akahisi ana akili timamu,kama hana mtindio wa akili basi atakuwa ni mtoto wa Akili MAVI,watu wana discuss jinsi ya kuweza kuisaidi Yanga yeye anaingiza khabari za kis***e oooh shaffih wewe ndo utakuwa umeandika hiyo makala hata kama shaffih ndo ameandika hilo haoni kama inaukweli ndani yake,mi longtime huyo Akili Mavi nilishamshtukia anatumiwa na watu kwanza siyo siri vizee vyote hivyo vya Yanga vinatumiwa na Manji na wala si mwingine,Inatakiwa ifike mahali wanachamaq wa Yanga waondokane na utumwa wa mawazo ule wa kutetemekea rangi nyeupe kwani Manji ana nini jipya mbona aliweza kuitelekeza Yanga alafu Kagame Yanga ikatwaa Kombe...Hata hivyo Manji kesha watu wanambabaikia ndo maana anawatumia watu kama hivyo Vijibabu visivyokuwa na mbele wala nyuma...kwanza huyo Akili Mavi sidhani kama hata ana-email address au anajuwa zungu lakuweza ku-communicate na Maximo ndo hapo TUNAPATA TAFSIRI YA AKILI MAVI ANATUMIKA...inamaana Yanga Sendeu keshafuzwa kazi mpaka huyo Akili mavi ana_press cnfrnc???sasa kama huyo M_sure anamamlaka ya kumfukuza mtu uwana chama basi haina sababu ya kufanya uchaguzi wa Mw/kiti na wkt Akili mavi yupo...Huyo akili mavi hapendi kukosolewa ndo maana anamind shaffih anapenda kusifiwa na baadhi ya watu wase**e wase**e kama Maulid Wakitenge.....Siyo siri wanaYanga TUZINDUKEEEEEEEEEE HUYO BWEGE HATUFAHI HATA KIDOGO,tukiendelea kumlelea TUTAKUJA KUPIGANA VIPANGE wenyewe kwa Wenyewe kwasababu ya Bwege Mmoja......Mi ni hayo tuu>>>>>>>>Alafu ww Washington nimekumind si kise**e..design Washington ww mmbeya mbeya flani ulikuwa unampigia simu mshikaji ili iweje?umtishie maisha au?
ReplyDelete,
Mtu mzima na mwenye akili timamu utamtambua hata kwa maneno yake,jamani hata kama ni suala la uhuru wa maoni,hebu tuyasahili maneno yetu kabla hatujayasubmit kwenye public plat form.
ReplyDeleteBaadhi ya comments zinamlaumu Shafii,lakini kwa akili ya kawaida who is shafii,yeye ni mwandishi anayo haki ya kuandika chochote kama mwandishi na kufanyiwa uhariri na kutolewa kwa jamii.Pili Yanga ni timu ya akilimali au ni ya wanayanga au tuseme ni ya wapenzi wote duniani wanaoipenda,Sasa yanga sio chama cha siasa ni club ya mpira wa miguu na inataratibu za kisoka zikiongozwa na taratibu za FIFA,na nia hasa ni kutoa burudani na kutoa ajira kwa wachezaji,Kwa maelezo hayo pale Yanga Akilimali yeye ni nani kwenye uongozi au yeye ni mmiliki wa timu ya Yanga,kwa sababu amekuwa kiherehere kwa kutumia utajiri wa mtu ,kwa kupitia huyu akilimali ndio mwanzilishi wa migogoro yote yanga.Na hao wasomi na wanachama wazuri waliopo yanga wasipokuwa makini kila siku yanga itakuwa vurugu pale mwenye pesa zake atakapoamua jambo na kumuita akilimali na kumpa pesa ya kahawa ili alianzishe
ReplyDeleteChukueni tahadhari wanayanga kabla ya hatari kubwa kutokea,ikiwa ni kutomruhusu huyo mmiliki feki (akilimali) kuisemea yanga,kwani yanga inamsemaji wake Lois Sendeu,
Mwisho hakuna kocha mzuri atakaye yumbishwa na waandishi wa habari,kwa kifupi misheni chafu iliyokuwa inaendeshwa na MANJI kupitia akilimali ya kumleta Maximo imefeli sasa wanatafuta kisingizio kwa kifupi Maximo anamkataba na klabu aliyonayo na wenzetu hawafanyi mambo ya kihuni kwa kuongea naye kwenye simu na kukurupuka na kuondoka kama wanavyoingia mikataba ya kumvizia mtu uchochoroni na kumsainisha na kusema huyu wa kwetu.Kwani ni lazima kuongea na uongozi husika wa timu aliyopo na watakapo kubaliana walipe gharama za kuvunja mkataba hapo ndio useme Maximo wakwetu,kwa hivyo wanayanga fungueni macho kwa jambo hili na sio kwa kumsingizia Shafii,Yanga mkifanya mzaha mnakula TANO tena kwani siasa imezidi hapo
SHAFII KEEP IT UP AND WELL DONE
KUTOKA KWA
Mpenda maendeleo ya soka Tanzania(TANZANIA KWANZA MIMI BAADAE)
Brother shafii haina haja ya wewe kwenda mahakamani kushitaki kwani kama mzee akilimali anasema uongo watu watajua hasipo onyesha ushaidi,hayo ndo mambo ya soccer,nikukumbushe juzi tu katika mchakato wa liverpool kutafuta kocha, mmiliki wa wigan alikuwa akitoa maneno mengi sana kuhusu liverpool but still liver hawakwenda mahakamani but walimuita jaa kuwa ni commedian,the same situation garry nevil anavyo ichambua chelsea pale skysports mpaka AVB alilamika still hawakwenda mahakamani,huyu mzee ndo alimvulia nchunga kofia yanga wa kala 5 chunga asikuvulie na wewe,cha muimu wewe hachana nae na umuone kama comedian.
ReplyDeleteSometime shaffih nayeye anakurupuka kuandika vitu.hawezi kukaa chini na kuandika kitu in a sense kwamba kisionyeshe ushabiki wake...siku zote anaandika uozo kuhusu yanga au arsenal bt when it comes to simba na Man u inakuwa tofauti..kimsingi mi ningekuwa mzee akilimali nisingemuomba msamaha ningemchana tena,atwambie kama hii website ni tawi la simba au man u tujue moja
ReplyDeleteEMBU WAANGALIE HAO WALIOMZUNGUKA, KUNA ANAEONESHA DALILI ZA KWENDA SHULE HAPO? NI WASWAHILI WATUPU,WANAOISHI MJINI KIMAGUMASHI.
ReplyDeleteMwacheni mzee wetu...mnaona timu inaanza kufanya vizuri mnataka kuweka mambo yanayoleta uchochezi..sisi we are fine with that mzee akilimali sisi hatuchagui rangi ya paka ili mradi anakamata panya..why bother with people that doesn't conern u huyo faraja asijidai ni mshabiki wa yanga ni mzushi tu mmoja wa simba asiyeitakia yanga mema..huyo mzee akilimali ameishabikia yanga hata wewe hujazaliwa kwa hiyo anaijua in and out..Tumeangalia timu kama arsenal chairman wake hillwoood yeye ni third generation ya kuwa chairman kutoka kwenye familia yake..lakini watu bado wanamuheshimu coz he loves arsenal. kwa hiyo kwangu mimi as long as huyu akilimali anaipenda yanga na yanga inafanya vizuri he has my full surppot. SHAFFIH UNATUMIKA KUIHARIBU YANGA BE PROFFESSIONAL PLEASE ACHA UNAZI UTAKUHARIBIA CARREER YAKO.
ReplyDelete