Search This Blog

Tuesday, June 19, 2012

BREAKING NEWS: BONIFACE MKWASA AJIUZULU UKOCHA TWIGA STARS

Mkwasa

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu leo.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkwasa anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo itolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Mapema baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki fainali za Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.

1 comment:

  1. Nakupongeza kwa hatua uliyofikia coz tumeshuhudia viongozi wengine mpaka watu wapige makelele na watishiwe maisha ndio wanajiuzulu.umefanya uungwana sana.hata hivyo tatizo la twiga stars sio kocha peke yake ni tatizo la kimfumo.wachezaji wanaokotwa tu mitaani hakuna ligi inayoeleweka ya mabinti hawa.TFF hebu mwaka huu anzisheni ligi ya wanawake ili siku za mbele tupate timu nzuri.pia nawapongeza mabinti hawa kwa kujituma kwa ajili ya taifa lao japo wanakutana na matatizo mengi.

    Nawasilisha.

    H.sato

    ReplyDelete