Search This Blog

Saturday, May 12, 2012

VITUKO VYAENDELEA SUDAN: SIMBA WANYWESHWA CHAI YA MAZIWA YA NGAMIA


WACHEZAJI wa Simba walijikuta wakinywa chai iliyotengenezwa na maziwa ya ngamia juzi Alhamisi lakini Emmanuel Okwi na Shomari Kapombe walishituka na kunywa chai ya rangi.

Simba ikiwa Khartoum ikijiandaa na safari ya kwenda mji wa Shandy, ilifikia katika hoteli ya Sharga ambako ndio walikunywa chai hiyo ya maziwa ya ngamia.

Tangu Simba ilipotua Sudan, Jumatano iliyopita, wachezaji wake wamekuwa wakipata shida na chakula cha Sudan.

Huku baadhi ya wachezaji wengi kama Felix Sunzu wakila mikate na mayai ya kukaanga na chai maziwa ya ngamia, Okwi na Kapombe wao waliagiza chai ya rangi.

Chai ya maziwa ya ngamia ndio inanyweka zaidi nchini Sudan kutokana na kutopatikana maziwa ya ng'ombe, ambao ni nadra sana Sudan kwa kuwa eneo kubwa la huko lina ukame na kufanya upatikanaji wa majani ya kulishia mifugo kuwa mgumu.

"Sijawahi kunywa maziwa ya ngamia," alisema Okwi, ambaye sambamba na Kapombe walimtaka mhudumu wa hoteli awapelekee chai isiyokuwa na maziwa.

Maziwa ya ngamia yanapatikana kwa wingi Sudan na hutumika kwenye chai katika hoteli na migahawa mingi ya Sudan. Ngamia wako wengi Sudan kutokana na nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1956 kuwa na eneo kubwa lenye ukame.

2 comments:

  1. kaka hapa Sudan ngamia ni kawaida, ni nyama hapa kama mbuzi au ng'ombe back home. Maziwa ya ngamia ni Sudan yote, siyo njama kwa hilo,ndio tamaduni zao. Hata ukienda kenya maeneo ya Isihoro wanakula ngamia na maziwa yangimia wanayanywa kama kawaida...ni hilo tu. Simba wenyewe wenyewe wanatakiwa kuwa focus, hapa mjini ni kina Samatta wanakipiga leo, na baadhi ya wabongo wachache tunaenda kuwaona...huko walipo Simba ni mbali bwana...usafiri wenyewe ni shida tupu.

    ReplyDelete
  2. Hapo hakuna hujuma, tuseme ukweli ndugu zangu. Nina uhakika hata Wasudan walipokuja Bongo haingekuwa rahisi kupewa chakula ambacho kinapatikana kwao na wamekizoea. Yaani tusiweke hamira kabisa, tunawaonea! Kumbukeni kuwa ukichanganya uongo na ukweli kwa ujumla wake kila kitu inakuwa uwongo.

    Nimefurahi kuona kuwa angalau wamepata uwanja, na muhimu zaidi waweze kufanya mazoezi. Kamwe timu isilegeze mkia kutegemea huruma ya CAF kwa vituko vya hapa na pale.

    Simba ni Taifa kubwa, tubane mkia uwanjani badala ya kupiga pelepeche - hivyo vitendo vichafu vya kweli iwe chachandu ya kuwabamiza zaidi! Inabidi kesho kubana mkia kwelikweli na kuachama kinywa ili kuwatafuna hao waarabu.

    ReplyDelete