Search This Blog

Friday, May 11, 2012

TP MAZEMBE NAO YAWAKUTA YA SIMBA -WAFANYIWA VITIMBI NA AL MERREIKH - GARI LAO LASHAMBULIWA NA RISASI

Utaratibu wa timu za kisudani kuzipokea vibaya timu pinzani zinapoenda kucheza nchini kwao umeendelea, baada ya Simba sasa ni TP Mazembe ambao jana mashabiki wa klabu ya Al Merreikh ya Sudan wameufanyia fujo msafara wa klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Khartoum, wakidai na wao walipokewa vibaya na klabu hiyo mjini Lubumbashi wiki mbili zilikzopita.
Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ipo Khartoum kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Merreikh, hatua ya 16 Bora.
Katika vurugu hizo, basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Mazembe limevunjwa vioo na athari zaidi ikiwemo hali hali za wachezaji bado hazijajulikana.
Sasa mechi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Omdurman, hatima yake ipo mikononi mwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)- ambayo inatarajiwa kuchukua hatua muda mfupi ujao, kubwa zaidi ikitarajiwa kuifuta mashindanoni Merreikh na kuifungia hivyo Mazembe kusonga mbele.







No comments:

Post a Comment