Search This Blog

Saturday, May 12, 2012

RAUL AIOKOA TIMU YAKE YA UTOTONI KUFILISIKA

Raisi wa klabu ya San Cristobal del los Angeles, Pedro Albares Iniesta, amesema leo kwamba klabu hiyo imenusurika kufilisika na kuvunjika kabisa kutokana na mchango wa £4,000 kutoka mchezaji wa zamani maarufu kabisa katika historia ya klabu hiyo, Raul Gonzales Blanco.

Mshambuliaji huyo alikaa na klabu hiyo miaka mitatu kabla ya kujiunga academy ya Atletico Madrid  mwaka 1990 na baadae kuhamia Real Madrid.

Klabu ya San Cristobal ilitangaza wiki kadhaa zilizopita kwamba wanahitaji kupata kiasi cha £4,000 kabla ya mwisho wa June ili kuweza kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kuwepo  - na hapo ndipo mchezaji wao wa zamani alipokuja kutoa msaada.

"Nimetaarifiwa kwamba fedha kutoka kwa Raul zimeshatumwa na na kila kitu kimekaa sawa sasa,: Iniesta alisema jana Alhamisi.

"Raul anamaanisha kila kitu hapa. Lakini tumemuomba kitu kimoja kingine : tunataka aje hapa siku moja tumkumbatie na tuongee na kumkumbusha siku zile za zamani...."

No comments:

Post a Comment