Search This Blog

Thursday, May 17, 2012

PICHA: ANGALIA JINSI WACHEZAJI WA SIMBA NA YANGA WANAVYOMLILIA MAFISANGO



Haruna Moshi 'Boban' akiwa na simanzi baada ya kifo cha mwenzake.
Emmanuel Okwi (kulia) nae alifika Muhimbili baada ya tukio hilo.
Uhuru Seleman wa Simba akilia kwa huzuni baada ya kufika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 
Kiungo wa Yanga na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima akiwa na majonzi kwa kifo cha mwenzake anayetokea Rwanda pia.
Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa (kushoto) pamoja na Uhuru Seleman wakimlilia mchezaji mwenzao.
Kiungo wa Simba, Patrick Mafisango ‘Mutesa’, amefariki leo alfajiri katika ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya Chang’ombe maeneo ya Chuo cha Ufundi, Veta, jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu uliushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umetapakaa damu nzito ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mchezaji huyo alipata ajali hiyo akitokea Klabu ya New Maisha kuelekea nyumbani kwake ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili T 387 BMZ kulikuwa na wenzake watatu ambao wote walitoka salama kwenye ajali hiyo.
(PICHA:RICHARD BUKOS/GPL )

1 comment:

  1. dah sio siri hapa limepotea djembe...........nimeamini kifo hakina huruma na huwezi kujua saa wala siku...

    ReplyDelete