Search This Blog

Tuesday, May 22, 2012

OFFICIAL: CHELSEA YATHIBITISHA DROGBA ANAONDOKA CHELSEA

Hatimaye klabu ya Chelsea imethibitisha rasmi kwamba Didier Drogba ataondoka klabuni hapo mwezi ujao.
Drogba ametumia miaka nane kuichezea Chelsea pale Stamford Bridge huku akishinda kila kombe kombe kubwa alilowhi kushiriki na timu hiyo.

Drogba alisema: "Nataka kummaliza maneno na tetesi zore, nathibitisha kwamba naondoka Chelsea.
"Umekuwa ni uamuzi mgumu sana  kwangu na nina jisikia fahari kwa yote niliyofanikiwa kuayapata hapa, nafikiri sasa ni muda sahihi kwenda kupata changamoto mpya.
"Nimeisadia timu yangu na tumeshinda kila kombe ambalo tumewahi kulishindania. Siku ya jumamosi ilikuwa maalum sana kwa kila mtu pale klabuni na kwa mashabiki wote na nina furaha kuwemo katika kikosi kilicholeta makombe kwenye klabu hii - ambayo imekuwa ndio nyumbani kwangu kwa takribani miaka nane.
"Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru kila mtu katika klabu hii hasa Roman na wachezaji wenzangu ambao wengi wao wamekuwa marafiki zangu wa karibu sana na watabakia kuwa hivyo milele. Pia ningependa kuwashukuru mashabiki wa Chelsea ambao siku zote walinifanya nijihisi wa kipekee kwa mapenzi walionionyesha.
"Naitakia klabu kheri na kuendelea kupata mafanikio mbeleni - siku zote mraendelea kuwa moyoni mwangu." - alimaliza Dider Drogba.

No comments:

Post a Comment