KIUNGO wa timu ya Taifa Nurdin Bakari ataukosa mchezo wa kimataifa dhidi ya Malawi baina ya timu hizo utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dae es Salaam,
Hatua hiyio inafuatia nyota huyo kutoka Yanga kuchanika nyama za paja wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo hali itakayomlazimu kuwa nje ya dimba kwa wiki moja.
Stars imepiga kambi kwenye hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo wake huo ikiwa ni mahususi kwa maandalizi ya mechi yao dhidi ya Ivory Coast kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia, utakaopigwa juni 2.
No comments:
Post a Comment