Search This Blog

Friday, May 4, 2012

NELFI IBANEZ: KOCHA WA KWANZA KIKE KUFUNDISHA SOKA WANAUME DUNIANI





"Changamkeni, onyesheni nguvu! Msisimame, zidisheni presha!" Sauti ya kike kutoka kiwanja kimoja pale Lima, ikiwasisitiza wachezaji wa kiume kuongeza bidii na kufanya mazoezi zaidi.

Nelfi Ibanez ni kocha wa kike nchini Peru akiifundisha klabu ya Hijos of Acosvinchos inayocheza kwenye level ya semi-proffessional.

Timu hii chini ya Ibanez imekuwa na rekodi nzuri ambayo imekuwa ikiwashangaza baadhi ya wadau wa soka duniani.

Ibanez, mwanamke wa kibolivia mwenye miaka 43, sio mgeni katika michezo. Kocha huyu mwenye nywele ndefu alianza kufundisha soka nyumbani kwao Bolivia na Spain - na amekuwa akitoa mafunzo kwa timu za vijana na klabu moja nchini Bolivia ambayo alishinda nayo mataji kadhaa katika ligi isiyokuwa ya kulipwa.

Anasema ndoto yake kubwa kawa sasa ni kuiwezesha klabu anayoifundisha ya Hijos of Acosvinchos kupanda mpaka kwenye ligi kuu ya Peru - ingawa anasemabado anajihisi mpweke katika soka.


"Ningependa kuwe na makocha wengi wa kike katika soka," Ibanez aliambia shirika la habari la AFP. "Nafikiri naweza nikawa peke yangu katika dunia. Katika nchi ambazo nimetembelea nilijikuta ni mwanamke pekee ninayefundisha soka wanaume. Hata timu za wanawake katika nchi kama Ujerumani, Marekani na Japan zinaongozwa na wanaume."

Kwa wakurugenzi wa Hijos, klabu iliundwa miaka 66 iliyopita katika mji mkuu na wahamiaji kutoka kijiji cha Andean huko Ayacuncho, Ibanez alikuwa ndio chaguo sahihi.

"Kulikuwa na makocha zaidi ya 20 wa kiperu wakitakata nafasi ya kuikochi timu hii, lakini baada ya kuangalia CV ya huyu mwanamke  - akiwa amesoma Bolivia, Paraguay, akifanya kazi FIFA na pia FC Barcelona - hatukufikiria mara mbili kabla ya kuwasiliana na wakala wake." alisema raisi wa klabu hiyo Jaime Gonzalez.

Ibanez anapenda kutumia mfumo wa kushambulia wa 4-3-3 au 4-4-2, akiwa na mipango ya kuweka presha kubwa katika nafasi zote za wapinzani.

"Kupaki basi nyuma kunaondoa ladha yote ya soka. Siamini katika mifumo hii," alisema  Ibanez.

Ibanez ni maarufu sana katika nchi ambayo wanawake bado wanatafuta uhuru wa kutoa sauti zao zisikike.
Lakini hajioni yeye kama mpiganaji sana. Alikuwa tu anapenda soka tangu akiwa mdogo.

"Sijui kama nimekuwa mpiganaji au shujaa sana. Imetokea tu kwangu," alisema.

Ndoto yake kubwa ni kuifundisha timu ya taifa ya Bolivia na siku moja awawezeshe kushiriki katika kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu World Cup ya 1994.

Anasema japokuwa amekuwa akitukunwa sana na kusikia maneno mengi machafu ndani ya uwanja lakini hajali.

"Wanaweza kusema chochote watakacho. Ni haki yao. Binafsi siku zote nimekuwa nikijiheshimu sana, kama wachezaji."


Wachezaji wa timu yake siku zote wamekuwa wakifanya mazoezi chini ya uangalizi wa mwanamke huyu bila kumuonyesha dalili zozote za ubaguzi.

"Huyu mwanamke anajua soka kiundani sana," alisema Yetro Garcia, kijana wa miaka 21 anayecheza kama mshambuliaji. "Kocha wetu ni shujaa sana na anapenda sana kushinda. Anajua kabisa nini anataka na jinsi ya kutuongoza."

"Sioni tofauti yoyote na kocha wa kiume," anazungumza Diego Moron. "Sina tatizo na yeye kuwa kocha. Kiukweli nafikiria ni jambo zuri sana."

Ibanez anasema amekuwa akipatwa na aibu kwa muda mrefu wakati wachezaji wa kiume wakiwa wanabadilisha nguo vyumbani.
"Hilo ndio tatizo lakini mara zote nimekuwa nikijishughulisha na speech yangu ya kiufundi na maelekezo mbele ya mechi," alisema.

Msaidizi wake Cesar Vidal, 56, alimuongelea pia bosi wake.
"Tunaongea lugha moja. filosofi moja ya kushambulia na kuufanya mpira uwe na ladha, tunaenda kuchukua ubingwa na kuipandisha timu yetu ligi kuu." 

No comments:

Post a Comment