Siku chache baada ya mshambuliaji wa kutumainiwa wa Villa Squad Nsa Job kujiunga na coastal union baadhi ya wanachama wa Villa Squad wameanza kumshutumu mwenyekiti wa klabu hiyo Bw Ramadhan Uled kwamba ndiye aliehusika kumuuza mchezaji huyo kwa dau la shilingi million kumi (10 Mil).
Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu hiyo anasema ameanza kupokea kauli za vitisho kitu ambacho si ustaarabu aidha alisema taarifa zozote zinazohusiana na transfers ni vema watu waulizie katika secretariet ambayo ipo chini ya Katibu mkuu Frank Mchaki na siyo kukurupuka.
Nsa job alikiri kumwaga wino Coastal Union baada ya msimu mzuri akiwa na Villa Squad kwa kuifungia mabao 12 katika ligi ya Vodacom, Nsa job alikusema haoni dhambi kumwaga wino katika klabu ambayo ana mahusiano nayo mazuri kama vile Villa Squad baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika bila kuweka wazi mkataba wake mpya umewagharimu wagosi wa kaya kiasi gani na kuzidi kusisitiza kwamba aliitumikia Villa kwa moyo wake wote bila kujali maslahi ndani ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment