Search This Blog

Wednesday, May 30, 2012

KALI YALEO: WAZIRI MKUU WA ITALIA ATAKA SOKA LIFUNGIWE MIAKA 3 ILI KUMALIZA RUSHWA - SHIRIKISHO NA VILABU VYA SERIE A VYAMPINGA

Shirikisho la soka nchini Italy (FIGC) na klabu kadhaa nchini humo wamekataa pendekezo la Waziri Mkuu wa nchini, Mario Monti, kwamba soka la kulipwa itabidi lisimamishwe kwa maiak 2 au 3 ili kuweza kumaliza kabisa skendo ya upangaji matokeo.

"Inasikitikisha sana wakati dunia ambayo inabidi iwe kielelezo cha maadili mazuri - michezo, ujana, ushindani, na usawa - unakuja kuwa na mambo ya uongo na kutia aibu," Monti alisema alipokuwa ameenda kumtembelea waziri mkuu wa Poland  Donald Tusk.

Lakini shirikisho la soka la Italia kwa haraka lilikataa wazo la Waziri mkuu Monti.
"Naelewa jinsi suala hili linavyoitia aibu Italia. lakini kusimamisha mchezo huu kutaaminisha ni kutoutendea haki mchezo wa soka, kwa kuwa jambo hilo likifanyika itakuwa sawa na kuwaadhibu watu wengi wanaocheza mchezo huu kwa haki na usawa na kuwaacha bila kazi. Hilo sio suluhisho."

Watu wa vilabu pia hawakuwa nyuma kumpinga waziri mkuu.

"Kabla hajasema inabidi tusimame kucheza soka inabidi aanze kuangalia matatizo yake na kila kitu anachokiharibu na kuvifunga na sheria zake," alisema Maurizo Zamparini, Raisi wa Palermo.

"Monti anaonyesha kutokujua kwake mambo vizuri kwa sababutimu za soka la kulipwa zinalipa euro millioni 800 kwa nchi hii kila mwaka."

No comments:

Post a Comment