Search This Blog

Thursday, May 31, 2012

HUYU NDIO KOCHA MPYA LIVERPOOL - AMRITHI KENNY DALGLISH

Rodgers akiwa na Kenny Dalglish
Utafutaji wa kocha wa Liverpool hatimaye umefikia tamati baada ya Brendan Rodgers kukubali kujiunga the Merseyside club kwa mkataba wa miaka mitatu kuiongoza klabu hiyo ya Anfield.

Rodgers atatangazwa rasmi kumrithi Kenny Dalglish ndani ya masaa 24 yajayo baada ya kumpa taarifa mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins kwamba anataka kuhamia Anfield.
Na moja ya kitendo cha kwanza anachoweza kukifanya ni kumsaini Gylfi Sigurdsson, ambaye bado hajafanyiwa vipimo vya na afya na Swansea ili kukamilisha uhamisho wake wa £8 million kutoka Hoffenheim.

Liverpool itabidi wailipe fidia inayokadiriwa kufikia £5million ili kuweza kumpata Rogders.

Rodgers aliongea na maofisa wa Anfield jana jumatano, akiwemo mwenyekiti Tom Werner, baada ya Swansea kuwapa ruhusa ya kuongea na kocha huyo juzi jumanne - na bado ya mkutano huyo Rodgers alienda Wales kumwambia Jenkins kwamba ataondoka Liberty Stadium kuelekea Anfield. 


No comments:

Post a Comment