Search This Blog

Friday, May 11, 2012

KALI YA LEO: MMILIKI WA KAMPUNI YA KUBETI KUPOTEZA £500,000 CITY WAKICHUKUA UBINGWA.

Mwaka 1998, muasisi na mmiliki wa kampuni ya kubeti(wazee wa kuweka mizigo) Fred Done alipoteza £500,000 kwa kuweka mzigo au kubeti mapema kwamba Manchester United watachukua taji la Premier League wakati timu hiyo ilipokuwa ikiongoza kwa pointi 12 mbele ya Arsenal - lakini baadae Arsenal wakaiifikia United na kuwazidi kwa pointi moja na kutwaa ubingwa.

 Done ambaye alikuwa ndio mtu wakwanza kutoa kucheza kamari mapema katika mbio za ubingwa za msimu huo na ungeweza kufikiri labda angejifunza, lakini haikuwa hivyo.

Mwezi uliopita, Bwana Done ambaye ni shabiki mkubwa wa Man United - alilipa kiasi cha £500,000 kwenye kubeti kwamba klabu yake anayoipenda itachukua kombe tena. Done alikaririwa akisema hivi kwenye mtandao wa twitter.

"Hata bado kukiwa kuna Manchester Derby na huu uongozi wa pointi tano ni vigumu sana kwa City kutupiku, hivyo kwa mara nyingine tena naweka mzigo wangu mapema kwa United kiasi cha nusu millioni paundi.
"Mwaka 1998 baada ya Arsenal kuchukua ubingwa Fergie aliniambia nisirudie tena kuweka fedha zangu mapema lakini Sir Alex hahitaji kuwa na wasiwasi, siwezi kukosea tena mara hii, United kwa hakika watabeba ndoo msimu huu."

Lakini kama ambavyo baadhi ya wafanyakazi wa United wanavyosema kwamba kamwe usiudharau ushauri wa Sir Alex Ferguson. Mambo yamegeuka City wamepangua uongozi wa pointi 5 za United na sasa jumapili wanaweza kubeba ndoo na kumfanya bwana Fred Done kupoteza zaidi ya billioni moja za kitanzania kwa mara nyingine tena ndani ya miaka 12.

Ili bwana Done aepuke hasara hiyo inabidi QPR wapate matokeo ya chanya dhidi ya City na United washinde mechi ya dhidi ya Sunderland na kubeba ubingwa wa 20 wa EPL.

No comments:

Post a Comment