Search This Blog

Friday, May 4, 2012

JULIO: TOTO WASUBIRI KIPIGO TU


KLABU ya Coastal Union iko katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mechi yao ya kumalizia msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Toto Africa inayotarajiwa kupigwa dimba la Mkwakwani jijini hapa.
Akizungumza jijini hapa juzi, Kocha Mkuu wa Wagosi wa Kaya, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, alisema wameamua kuanza maandalizi ili kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu muhimu kwenye mechi hiyo.
Kihwelu alisema kutokana na uimara wa kikosi chake ambacho kimekuwa tishio kwa baadhi ya timu kongwe zinazoshiriki ligi hiyo, wana imani kubwa ya kuibuka na ushindi wa kishindo wakiwa nyumbani.
“Ninachoweza kusema ni kuwa mechi hiyo haitusumbui akili, kwani tuna imani kubwa na kikosi chetu kuweza kushinda siku hiyo,” alisema Julio.
Kocha huyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo, ili kuwapa hamasa wachezaji kufanya vizuri.

1 comment:

  1. Kaka Jamhuri Kihwelu "Julio" endeleza mapambano, kaza buti, ninaamini kwa uwezo wako, ushirikiano mzuri toka kwa viongozi, wanachama, wachezaji na wadau wa kandanda unaweza kabisa kuionoa, kuivusha Coastal Union na pia kuleta mapinduzi na maendeleo makubwa katika soka hapa Tanzania. Ninakutakia mafanikio mazuri.

    ReplyDelete