Search This Blog

Saturday, May 26, 2012

ETOO KUTUMIA MAMILIONI YA WARUSI KUFUNGUA KITUO CHA SOKA KENYA


MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya taifa yCameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Samuel Eto'o, amekiri kuipenda Kenya hasa maeneo ya Pwani.

Eto'o amesema hayo baada ya kutangaza kuanzisha Chuo cha Soka katika eneo la Laikipia na kununua majumba kadhaa mjini Mombasa.


Mwanasoka huyo pia amezuru Laikipia kutazama mechi ya fainali ya Kombe la Laikipia Unity ambalo linafadhiliwa na Wakfu wa Zeitz.


Etoo alitangaza azimio la kuanzisha chuo hicho baada ya kuwaona wanasoka chipukizi walivyo na vipaji vya soka.
Kenya ina vipaji chungu nzima katika soka na chuo chetu kitasaidia kuwakuza na kuwapa vijana nafasi ya kujipatia riziki, kitaifa na kimataifa pia.

Etoo pia alisema anavutiwa mno na mandhari ya Mkoa wa Pwani akidokeza kuwa na nia ya kutafuta mali katika eneo hilo.

Ninaipenda Kenya na kila ninapokuja ninahisi kuwa nyumbani. Ninatamani kujenga au kununua nyumba mjini Mombasa lakini Laikipia pia ni kuzuri, alisema mwanasoka huyo.

1 comment:

  1. Ngoja na sisi tumwalike Drogba aje awekeze, tutamuuliza naye kama anapenda ukanda wa pwani tutampa eneo la Kigamboni au kama hapendi maeneo ya pwani tutampelekea ukanda wa savannah Shinyanga.

    ReplyDelete