Kiungo wa Chelsea na England Frank Lampard amefeli kuweza kupona majeraha yake ya paja na ameondolewa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Euro 2012 nchini Poland na Ukraine.
Lampard, 33, alipata majeraha hayo kwenye mazoezi jana na alipewa taarifa mbaya na jopo la madaktari kufuatia vipimo alivyofanyiwa mapema leo.
Kiungo wa Liverpool aliyekuwa na msimu mbovu Jordan Henderson atambadili Lampard kwenye kikosi cha Roy Hodgson.
Jordan Henderson |
"Hodgson alisema: "Ni pengo kubwa sana kwa timu, tena hasa baada ya kumpoteza mchezaji mwingine Gareth Barry. Ukweli ni kwamba madaktari wameshindwa kutoa uhakika kwamba Frank anaweza kucheza kwenye mechi yoyote ya hatua ya makundi - hivyo ikabidi tumbadilishe na Henderson kwenye eneo la kiungo.
"Pamoja na kuwa ni pigo kwa timu na kwangu binafsi, pia namuonea huruma sana Frank mwenyewe . Amekuwa kwenye kiwango kizuri kuelekea kwenye michuano hii. Alitoa mchango mkubwa sana katika hatua za kufuzu kwenye Euro, kwa maana hiyo ni jambo la kikatili sana kutoweza kucheza kwa sababu ya majeruhi."
Ni habari za kuzuhunisha sana kwa England, ambao tayari walishawapoteza viungo wao muhimu Gareth Barry ambaye alipata majeraha ya tumbo kwenye mechi ya jumamosi dhidi ya Norway. Three Lions pia tayari ilishamkosa kiungo wao Jack Wilshare - ambaye alikosa msimu mzima uliopita kutokana na majeraha - huku kukiwa kuna mashaka juu ya ufiti wa Scott Parker.
No comments:
Post a Comment