Search This Blog

Tuesday, May 22, 2012

BASTIAN SCHWEINSTEIGER AJITETEA NA KASHFA YA KUKATAA KUMPA MKONO RAISI WA UJERUMANI



Mchezaji wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger ambaye siku ya jumamosi aligoma kumpa mkono Raisi wa Ujerumani wakati akipokea medali ya ushindi wa pili baada ya mchezo wa fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya dhidi ya Chelsea, leo hii amejitetea kwa kusema haikuwa dhamira yake kumfanyia kitendo kile Raisi wa taifa hilo.

Schweinsteiger ambaye ndio mchezaji aliyekosa penati ya mwisho ya Bayern katika mchezo ule, anasema wakati anaenda kuchukua medali ile hakuwa swa kiakili, alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na hata hakumbuki namna alivyofika pale juu, anasema ni uchungu wa kukosa penati ambayo iliikosesha ubingwa wa timu yake.

No comments:

Post a Comment