Search This Blog

Thursday, May 24, 2012

BAADA KUONGEZWA MKATABA - MILOVAN KUWATAJA WATAKAOACHWA NA SIMBA LEO


WAKATI mabingwa wa Soka Tanzania bara, Simba SC wakimuongezea mkataba kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Circovic  wachezaji wa timu hiyo watakaoachwa kwenye usajili msimu huu watajulikana kuanzia leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga pazia hilo la usajili litafunguliwa na kocha Milovan ambaye atapendekeza majina ya wachezaji watakaotemwa msimu huu.

Kamwaga alisema Simba ilikuwa inahitaji kukamilisha kwanza suala la mkataba mpya wa kocha Milovan aliyeiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania bara msimu huu ndipo waanze zoezi la usajili.

"Kocha wetu alikuwa na mkataba wa miezi sita ambao umemalizika hivi karibuni, leo hii (jana) mchana Kamati ya Utendaji tupo kwenye  mchakato wa kumsainisha kocha Milovan mkataba mpya.

"Baada ya kusaini mkataba huo kocha atapendekeza majina ya wachezaji watakaobaki zoezi litakaloanza kesho 'leo' alisema Kamwaga na kuongeza kwamba kocha huyo atashirikiana na benchi zima la ufundi la timu hiyo.

Kimwaga alisema wapenzi na mashabiki wa timu hiyo watarajie usajili mzuri msimu huu ambao utaiwezesha timu yao kufanya vizuri  ndani na nje ya nchi kama walivyofanya msimu huu.

No comments:

Post a Comment